Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
Wamiliki wa shule binafsi wameaswa kuacha kuwarubuni wazazi kwa kuwataka kuwalipia ada watoto kwa ajili ya kuwafundisha masomo ya ziada kipindi cha likizo.
Hayo yamesemwa leo Aprili 14, 2025 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, wakati akifungua rasmi mkutano wa 35 wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo mkoani Morogoro, na kutoa wito kwa watumishi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo Toleo la 2023.
"Kuna wakati shule zinaongeza muda wa kukaa shuleni kwasababu pengine kuna uhaba wa walimu, kwahiyo ule muda wa kufunga shule wanafikiria tuongeze muda kidogo tufidie masomo ambayo hayajafundishwa lakini kwa shule inayotangaza kwamba wazazi sisi shule yetu ina walimu wa kutosha, walimu walio bora kabisa halafu wazazi wanaleta wanafunzi kwenye shule hiyo na inaposhindwa kuwaachia wanafunzi kwenda likizo inaonekana kuna kitu waliwadanganya wazazi, "amesema.
Amesema karenda hiyo imeandaliwa kuhakikisha kwamba wakati wa kusoma kwa muda uliopangwa kutamaliza kila kitu na wanafunzi lazima wasome kwa masaa yale ya kila siku sio kulazimishwa kukaa na wakati wa likizo kuambiwa wasiende nyumbani.
"Kamishna ndiye anayetoa karenda ya ufundishaji anasema masomo yataanza tarehe ngapi, kutakuwa na likizo lini, shule zitafunguliwa lini na karenda ile ni ya mwaka mzima na waraka wa Kamishna ni waraka wa kimaraka
Prof. Mkenda amesema kuwa tabia hiyo ya baadhi ya wamiliki wa shule binafsi na walimu inazorotesha afya ya ufikiri kwa watoto na ndio maana wizara imepanga vipindi vya mapumziko kwa watoto, ili kuwapa ari ya kusoma pindi warejeapo likizo.
Aidha, amesema sera mpya ya elimu inalenga kuleta mageuzi ya kimfumo katika sekta hiyo kwa kutoa maarifa na ujuzi unaohitajika katika karne ya 21, kupitia makundi mawili ya elimu ambayo ni elimu ya jumla na elimu ya Amali, ili kumpa kila mwanafunzi fursa ya kuchagua njia inayomfaa kwa maisha na taaluma.