Breaking

Saturday, 19 April 2025

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WATEMBELEA BUSTANI YA WANYAMA YA 'JAMBO ZOO'

  

Na Kadama Malunde - Shinyanga

Waandishi wa habari katika Manispaa ya Shinyanga kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) wametembelea bustani ya wanyama Jambo Zoo iliyopo katika eneo la Ibadakuli, Mjini Shinyanga, inayomilikiwa na Kampuni ya Jambo Group.

Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2025 ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na kuwaunga mkono wawekezaji wazawa, ambapo imeratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mhifadhi wa Jambo Zoo, Babuu Burhan Kajuna, alisema bustani hiyo ina wanyama wa aina mbalimbali ambao wamepewa mafunzo na kuzoea binadamu, hivyo kuwawezesha wageni kupiga nao picha kwa ukaribu.
"Tunawashukuru waandishi wa habari kwa kutembelea Jambo Zoo. Tunawakaribisha wananchi wote waje kufanya utalii wa ndani hapa Shinyanga. Bei zetu ni rafiki kabisa – watu wazima ni shilingi 20,000= na watoto shilingi 10,000/=," amesema Kajuna.

Ameongeza kuwa wageni wanaofika katika bustani hiyo hupata fursa ya kujifunza kuhusu tabia za wanyama, kupiga nao picha kwa ukaribu, na kuwalisha chakula kwa mikono yao.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Chapa kutoka Jambo Group, Nickson George, amewataka wananchi kuitembelea bustani hiyo hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, wakiwa na familia zao, huku wakifurahia vinywaji vipya vya Jambo Lemon Lime na Jambo Power Boom.

Aidha, Mratibu wa ziara hiyo, Marco Maduhu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya SPC na mfadhili wa safari hiyo, ameipongeza Kampuni ya Jambo Group kwa uwekezaji wa bustani hiyo ya wanyama, akisema umeunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha utalii wa kupitia filamu ya The Royal Tour.

Bustani ya Jambo Zoo inaendelea kuwa kivutio kikuu kwa wakazi wa Shinyanga na wageni, ikiwa ni sehemu ya utalii wa elimu, burudani na uhifadhi wa wanyama katika mazingira salama na rafiki kwa familia.

PICHA NA KADAMA MALUNDE NA MARCO MADUHU👇
Mhifadhi wa Jambo Zoo Babuu Burhan Kajuna, akizungumza na waandishi wa habari ambao wametembelea Bustani hiyo ya Wanyama.
Msimamizi wa Chapa Jambo Group Nickson George akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameshika vinjwaji vipya ambavyo ni Jambo Lemon Lime na Jambo Power Boom, katika Tour hiyo ya Jambo Zoo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Marco Maduhu akielezea Tour hiyo ya JAMBO ZOO na namna alivyo anzisha wazo hilo ili kuunga mkono Juhudi za Rais Samia Kuhamasisha Utalii wa ndani na kuwa "Support" wawekezaji wazawa.
Waandishi wa habari wakiwa TOUR JAMBO ZOO.




Picha za pamoja zikipigwa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages