
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (katikati) akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (watatu kutoka kulia) akifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa usaili wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sang una wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Kamati yake iliyofanyika Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.

Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Viongozi na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kamati yake katika ofisi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Omar Kombo akiwasilisha hoja wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyofanyika katika ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye akiwasilisha mada kuhusu TEHAMA ilivyoboresha mchakato wa ajira wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Kaimu Naibu Katibu, Menejimenti ya Ajira, Bi. Somwana Manjenga akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu mchakato wa ajira wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho kuhusu mchakato wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakisikiliza maoni ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Na Veronica Mwafisi-Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kuzingatia maoni na ushauri unaotolewa na kamati hiyo ili kuhakikisha mchakato wa ajira unafanyika kwa ufanisi mkubwa na uwazi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Kamati yake wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza utendajikazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mhe. Dkt. Mhagama ametolea mfano maoni ambayo Kamati yake iliyatoa kuhusu usaili kufanyika katika ngazi za mikoa badala ya kuwalazimu waombaji kazi wote kufika jijini Dodoma kumeleta matokeo chanya kwa waombaji kazi hao.
Vilevile Dkt. Mhagama amezungumzia matumizi ya mfumo wa Ajira Portal kwa waombaji kazi kuondokana na dhana tofauti ya upendeleo wa kupata ajira katika Utumishi wa Umma.
“Mfumo wa Ajira Portal umeondoa dhana ya kuwepo kwa upendeleo kwa waombaji kazi, ninaamini wengi wamepata ajira serikalini pasipo kupitia kwa mtu yeyote.” amesema Mhe. Dkt. Mhagama.
Kwa Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameishukuru Kamati hiyo kwa kutoa maoni na ushauri mara zote ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kutekeleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kikamilifu.
Aidha, Naibu Waziri Sangu amewaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuendelea kuwa Mabalozi wazuri wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma ili kuwahakikishia wananchi kuhusu uwazi wa namna ajira katika Utumishi wa Umma zinavyopatikana kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Sekretarieti hiyo wakati wa kuomba kazi.
Akielezea mafanikio baada ya kutumia mfumo wa Ajira Portal, Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye amesema, kupitia mifumo wameweza kuajiri Rasilimaliwatu yenye uwezo wa kufanya kazi na kutoa matokeo chanya pamoja na kuondoa hoja za kuajiri kwa dhana ya upendeleo.