Breaking

Monday, 14 April 2025

RC MACHA AZINDUA MAGARI YA MRADI WA MAJI YA SH. MILIONI 276.9

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiwa katika moja ya magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amezindua rasmi na kukabidhi magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na maeneo ya Tinde, Didia na Iselamagazi katika Halmashauri ya Shinyanga.

Magari hayo yenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 276,950,000/- yamenunuliwa kupitia sehemu ya tatu ya mradi huo, ambayo inalenga kuimarisha uwezo wa taasisi katika usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mradi.

Magari haya yatawezesha usafiri wa haraka na wa uhakika kwa timu za usimamizi wa mradi, wakandarasi na wadau wengine wanaohusika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
Muonekano wa magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na SHUWASA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumatatu Aprili 14, 2025, Mhe. Macha amesema magari hayo yataongeza kasi na ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za mradi kwa timu za usimamizi, wakandarasi na wadau wengine wanaoshiriki katika kutoa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira.

"Kupatikana kwa magari haya ni hatua muhimu katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa mradi huu mkubwa. Tunatarajia kazi zifanyike kwa haraka na kwa viwango bora kwa maslahi ya wananchi," amesema Mhe. Macha.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada kubwa anazozifanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji safi na salama, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kampeni ya "Kumtua Mama Ndoo Kichwani."
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi na kukabidhi magari mawili mapya.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kazi kubwa anayofanya kupitia miradi ya maji nchini. Serikali inaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, na haya ni matokeo chanya ambayo wananchi wetu wanayaona na kuyaishi," ameongeza.

Vilevile, Mhe. Macha amewapongeza watumishi wa SHUWASA kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kuwataka kutumia magari hayo kwa matumizi yaliyokusudiwa huku wakihakikisha yanatunzwa ipasavyo na kufanyiwa matengenezo mara yanapoharibika.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanalipa ankara za maji kwa wakati ili kuiwezesha SHUWASA kutoa huduma bora zaidi.

"Mtumiaji wa maji analazimika kulipa ankara kwa wakati kulingana na matumizi yake. Na kwa watumishi wa SHUWASA, muwajibike kwa mujibu wa sheria na maadili ya kazi. Anayekengeuka awajibishwe, na yeyote atakayekamatwa akiiba maji, achukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria bila huruma," amesema Mhe. Macha.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola, amesema mradi huo unatekelezwa katika maeneo ya Tinde, Didia na Iselamagazi ndani ya Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi wa mazingira kwa wananchi.

“Mradi huu unafadhiliwa kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa gharama ya Euro milioni 76, ambapo Euro milioni 1 imetolewa kama ruzuku kwa Serikali ya Tanzania,” ameeleza Mhandisi Katopola.

Utekelezaji wa mradi mzima unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2028, na unahusisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya maji safi, ujenzi wa miundombinu ya usafi wa mazingira pamoja na kuimarisha uwezo wa taasisi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (katikati, akikata utepe wakati akizindua rasmi na kukabidhi magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Muonekano wa magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) 

Muonekano wa moja ya magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiendesha moja ya magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola funguo za magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na SHUWASA

Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akisoma taarifa ya Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na SHUWASA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi na kukabidhi magari mawili mapya yaliyonunuliwa kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaotekelezwa na SHUWASA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akipiga picha na wafanyakazi wa SHUWASA

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages