Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Ndg John Mongella ametoa sifa kwa jumuiya ya UWT kwa kuwa mstari wa mbele katika kuelezea kazi za Chama kwa wananchi kutokana na Jumuiya hiyo kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Cha kawaida Cha Baraza Kuu la UWT uliofanyika katika ukumbi wa NEC jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu Mongella amesema kwa Sasa Taifa linajiandaa na Uchaguzi Mkuu hivyo wajumbe wa UWT wanapaswa kushikamana na kushirikiana katika kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo.