Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Gérardine Mukeshimana, katika kikao cha pembezoni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu uliofanyika tarehe 2–3 Aprili 2025 mjini Berlin, Ujerumani.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ummy amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendeleza ushirikiano na IFAD katika kuimarisha miradi ya kilimo inayolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa maendeleo jumuishi.
Viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya maendeleo jumuishi ili kuhakikisha programu za kilimo zinakuwa shirikishi, zenye usawa, na zenye manufaa kwa jamii nzima.