Na; Mwandishi Wetu - DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (Mb) amekutana na kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini walipokutana nao (Siku ya Jumatatu Aprili 14, 2025) jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Katambi amewashukuru wajumbe hao na wananchi wa shinyanga kwa kumuamini na kumpatia fursa hiyo muhimu ya kuwakilisha hivyo ameahidi kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukuza Maendeleo ya wananchi wa mkoa huo.
Wageni hao wa Naibu Waziri Katambi watatembelea ukumbi wa bunge tarehe 15 Aprili, 2025 kwa lengo la kushuhudia zoezi la kuhitimisha uwasilishaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Anold Makombe na Katibu wa CCM Wilaya, Halima Chacha.