Breaking

Thursday, 10 April 2025

DEUS SANGU ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UONGOZI BARANI AFRIKA

 



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Sangu ameshiriki Mkutano wa 8 Kimataifa wa Jukwaa la Vongozi Africa (African Leadership Forum) unaoendelea kwa muda wa siku nne jijini Kampala, Nchini Uganda.


Mkutano huo umefunguliwa leo na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kagutta Museveni na umeshirikisha viongozi wakuu wa Nchi wastaafu na wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo mada kuu kwa mwaka huu 2025 ni juu ya hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) na kuweka mikakati kabambe itakayosaidia kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa malengo hayo hususani katika maeneo ya vita dhidi ya umaskini na kukuza uchumi wa bara la Afrika.


Pia katika Mkutano huo Washiriki watapata fursa ya kujadili masuala muhim kuhusu mustakabali wa Bara la Afrika katika nyanja za Elimu, Afya na pia juu ya suala mabadiliko ya Tabia Nchi.


 Akizungumza katika mutano huo, Mhe.Sangu amesema ili kutimiza malengo endelevu Barani Afrika (SDG's) kunahitajika mikakati maalum inayolingana na mazingira ya kila nchi.


Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa zinazolikumba bara la Afrika kwa ujumla kama vile mabadiliko ya tabia nchi, rushwa, idadi kubwa ya vijana wasio kuwa na ajira, na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi kwa nchi nyingi Barani Afrika.


Amesisitiza kuwa ili kukabiliana na hayo ni lazima kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa kuondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima ili kuleta mabadiliko chanya ambayo yatapelekea kupunguza changamoto hizo na kufanikisha malengo haya kufikia mwaka 2030



Mkutano huo, umehudhuriwa viongozi wandamizi kutoka nchi mbalimbali pamoja na Marais Wastaafu kutoka Bara la Afrika akiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Kikwete ambaye pia ni mlezi wa Jukwaa hilo la viongozi Barani Afrika, Rais Mstaafu Tunisia Mhe. Mohamed Marzouk, Rais Mstaafu wa Sierra Leone, Mhe. Ernest Koroma pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Boshe.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages