
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( kulia) akimkabidhi zawadi Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( kushoto) mara baada ya ziara ya kikazi.
.....
TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kushirikiana na Serikali ya Uswisi katika kufanya utafiti na ubunifu kama mkakati wa kukuza masoko ya kazi za tafiti na bunifu .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Arusha wakati wa ziara ya kikazi ya Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli, Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, Serikali hiyo imekuwa na ushirikiano wa karibu na NM-AIST katika miradi miwili ikwemo Kituo cha Mafunzo ya Kidigitali na Mradi wa Nishati inayotokana na mabaki ya mimea .
“Lengo kubwa la ziara ya balozi katika taasisi yetu ni kuona fursa zilizopo na namna ya kuendelea kushirikiana hasa katika eneo la sayansi, teknolojia na ubunifu, ukizingatia Uswisi wameendelea sana katika sekta hizi hivyo, ni fursa kwetu kujifunza na kujiunganisha na taasisi na kampuni kutoka huko ili kupata masoko ya bidhaa zetu” alisema Prof. Kipanyula
Ameongeza kuwa, eneo lingine la ushirikiano ni pamoja na wanasayansi wa Nelson Mandela kwenda uswisi huku Maprofesa wa uswisi kuja kufundisha na kufanya tafiti za pamoja kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kubadilishana uzoefu na ujuzi.
Kwa Upande wake Balozi wa Uswisi nchini Balozi Nicole Providoli amefurahishwa na fursa zinazopatikana NM-AIST na kuahidi kuendeleza ushirikiano, kwa kufanya kazi kwa pamoja katika kubadilishana ujuzi na uzoefu ili kuleta matokeo chanya katika teknolojia, ubunifu na sayansi.
Balozi Nicole Providoli alipata wasaa wa kutembelea Kituo cha Elimu ya Kidigitali ( C-CoDE), Maabara ya Nishati Endelevu ( Sustainable Energy Lab) .pamoja na Kituo cha Tehama chenye Komputa ya Kuchakata Taarifa kwa kasi kubwa (HPC).

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( kulia) akimkabidhi zawadi Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( kushoto) mara baada ya ziara ya kikazi.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( aliyenyoosha mkono kushoto) akielezea historia ya taasisi hiyo kwa Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kikazi.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( aliyesimama) akielezea kuhusu Nelson Mandela Radio kwa Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( kulia) wakati wa ziara ya kikazi.

Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( katikati aliyekaa) akiuliza swali namna kituo cha elimu kidigitali kinavyofanya kazi ( C-CoDE) kwa Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) wakati wa ziara ya kikazi na Kushoto ni Afisa Tehama wa kituo hicho Bw. Octavian Kanyengele.

Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( mwenye suti nyeupe) akipata maelezo kuhusu Kompyuta ya Kuchakata Taarifa kwa kasi kubwa ( HPC) kutoka kwa Afisa Tehama Bw. Mdoe Mwamunyange ( kulia) wakati wa ziara ya kikazi , wa kwanza kushoto ni Makamu Mkuu Taasisi ya Afrika Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula.

Prof. Maulilio Kipanyula Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Nicole Providoli ( mwenye suti nyeupe) wakati wa ziara ya kikazi.