Mkuu wa Idara ya Malipo wa Makao Makuu ya benki hiyo, Bw. Madaha Chaba akikabidhi viti vya waalimu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi katika shule ya msingi Nhobola.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi, Benki ya CRDB imekabidhi madawati 160 na viti 6 vyenye thamani ya Shilingi milioni 10 kwa shule mbili za msingi zilizopo wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika leo Aprili 11, 2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Nhobola na Mwamala, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, Mkuu wa Idara ya Malipo wa Makao Makuu ya benki hiyo, Bw. Madaha Chaba amesema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya benki katika kurudisha kwa jamii asilimia moja ya faida inayopatikana baada ya kodi.
“Tulipokea maombi kutoka kwa uongozi wa shule hizi kuhusu uhitaji wa madawati. Kama benki inayojali jamii, tuliona ni vyema kutoa mchango huu ili kusaidia watoto wetu kupata mazingira bora ya kujifunzia,” amesema Chaba.
Chaba amewahamasisha wananchi kuendelea kutumia huduma za Benki ya CRDB kwa kuwa zimeboreshwa na zinaendeshwa kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, ikiwemo utoaji wa mikopo nafuu na huduma bora za kifedha.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu David Mashauri amesema kuwa sekta ya elimu katika wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi kama vile uhaba wa madawati, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
“Msaada huu umetufariji sana, lakini bado tunahitaji mashirika na taasisi zaidi kuiga mfano wa CRDB ili kuboresha elimu kwa watoto wetu,” amesema.
Akipokea madawati na viti hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi ameishukuru Benki ya CRDB kwa moyo wa kizalendo na kupongeza juhudi zake katika kushirikiana na serikali kutatua changamoto za kijamii.
“Kupitia msaada huu, wanafunzi wetu sasa watakuwa na mazingira bora ya kujifunzia. Tunatoa rai kwa shule kuhakikisha madawati haya yanatunzwa vizuri ili yadumu kwa vizazi vijavyo,” amesema Mhe. Masindi.
Aidha, ameahidi kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu na taasisi kama CRDB katika kutekeleza miradi ya kijamii kwa manufaa ya wananchi.
Kwa upande wake, Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wagana ameeleza kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na jamii kwa kutoa asilimia moja ya faida yake kila mwaka katika kusaidia sekta mbalimbali kama elimu, afya na mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya viti na madawati vilivyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya msingi Nhobola.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wagana akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi meza na viti katika shule hizo.
Mkuu wa Idara ya Malipo wa Makao Makuu ya benki hiyo, Bw. Madaha Chaba akikabidhi viti vya waalimu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi katika shule ya msingi Nhobola.
Mkuu wa Idara ya Malipo wa Makao Makuu ya benki hiyo, Bw. Madaha Chaba akikabidhi viti vya waalimu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi katika shule ya msingi Nhobola.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya viti na madawati vilivyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya msingi Nhobola.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Nhobola akishukuru kwa kupatiwa madawati hayo na benki ya CRDB.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Nhobola akishukuru kwa kupatiwa madawati hayo na benki ya CRDB.
Madawati yaliyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya msingi Mwamala.
Madawati yaliyotolewa na benki ya CRDB katika shule ya msingi Mwamala.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kishapu Jenipher Juma akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Maganzo Kishapu Constansia Albinus akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano katika shule ya msingi Mwamala.
Wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Mwamala katika hafla hiyo ya makabidhiano.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wagana akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi meza na viti katika shule ya Msingi Mwamala.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi akikabidhi dawati kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mwamala.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi akikabidhi dawati kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu David Mashauri.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu David Mashauri akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati katika shule ya msingi Mwamala.
Diwani kata ya Ukenyenge Mhe. Anderson Mandia akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano shule ya Mwamala.
