Breaking

Monday, 17 March 2025

WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA VIPODOZI WATAKIWA KUSAJILI BIDHAA ZAO TBS

Machi 17 , 2025 Shirika la Viwango Tanzania TBS limewataka Wafanyabiashara na Wananchi kuuza na kununua bidhaa za Vipodozi zilizosajiliwa na Shirika hilo kuepuka madhara yanayosababishwa na utumiaji wa Vipodozi vyenye Viambato Sumu ambayo ni kama vile Kansa , Magonjwa ya Uzazi , miwasho , Saratani n.k.

Hayo yamesemwa na Afisa Viwango Mwandamizi TBS Bw.Alexander Mashalla wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Madhara ya matumizi ya Vipodozi vyenye Viambato Sumu , Mapema Leo hii Makao Makuu ya Shirika hilo Ubungo Jijini Dar Es salaam.

Bw.Mashalla amesema kuwa Kuna Viambato vinavyopatikana katika Vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku , viambato hivyo vimepigwa marufuku ili kulinda Afya za watumiaji kwani utumiaji wa Vipodozi vyenye Viambata Sumu huleta madhara ya Kiafya kama vile Madhara katika Ngozi , kusababisha Miwasho , kuleta makovu , madhara katika Mfumo wa Uzazi , Saratani , Kansa n.k

" Shirika la Viwango Tanzania linadhibiti na kusimamia ubora wa Vipodozi kwa mujibu wa Sheria ili kulinda Afya ya Watanzania, na katika kuifanya kazi iyo vipo Viwango vya vipodozi vinavyotoa mwongozo wa Ubora wa Vipodozi kwa kutumia kiwango TZS 638, na Mwongozo huo unatolewa kwa Wazalishaji na Waingizaji wa Bidhaa za Vipodozi namna gani wanaweza kutengeneza Vipodozi katika Ubora unaotakiwa .

Baadhi ya Bidhaa za Vipodozi zilizopigwa marufuku ni Carolite , Princess Cream, Viva Super Lemon Cream, Claire Cream, Movate Soap , Kiss Lotion na Vingine takribani 300 , kuona Orodha nzima ya Vipodozi hivi vilivyopigwa Marufuku kutokana na kuwa na Viambata Sumu tembelea Tovuti ya Shirika ya www.tbs.go.tz

Kwa upande wake Bw. Nicodemus Mahuma Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi TBS ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Bidhaa za Vipodozi kuhakikisha wanasajili Bidhaa zao TBS ili kulinda Afya za Watumiaji , na wito mwingine umetolewa kwa Wananchi kuhakikisha wanasoma na kuangalia Bidhaa hizo kabla ya kuzinunua , lakini pia kutembelea Ofisi au Tovuti ya Shirika hilo ambayo ni www.tbs.go.tz ili kupata taarifa zaidi

" Lakini pia kama Mwananchi hajaridhishwa au ana mashaka na Bidhaa ya Kipodozi husika au Bidhaa nyingine yeyote ile anaweza kupiga simu ya BURE ya TBS kupitia namba 0800110827 ili kupata msaada na maelezo ya Haraka " amesema Mahuma.

Aidha Bw. Mahuma amemalizia kwa kusema kuwa Shirika la Viwango limekua likijitahidi kutoa elimu juu ya Ubora wa Bidhaa hizo kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kutoa wito kwa Wananchi na Wafanyabiashara kuzingatia elimu hiyo .
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages