Na Mwandishi Wetu.
Machi 26 , 2025 Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) limewasihi Watumiaji mbalimbali wa Vifaa Tiba kuhakikisha wanapeleka Vifaa vyao TBS katika Maabara ya Taifa ya Ugezi ili kuhakiki Usahihi wa Vipimo wa Vifaa hivyo utakaowasaidia kuwa na uhakika wa majibu yanayotolewa na Vifaa hivyo suala litakalopelekea kujenga uaminifu na kulinda Afya za Wateja wanaowahudumia.

" Mfano katika Hospitali , Vifaa vinapokua vimefanyiwa Ugezi vitatoa majibu sahihi ya Vipimo ambayo yatamwezesha Daktari kujua mgonjwa ana tatizo gani na kuchukua hatua stahiki za kupambana na ugonjwa husika kwa haraka sana, *daktari hutoa matibabu kutegemea Majibu yaliyotoka maabara, hivyo kama maabara imefanyiwa ugezi daktari atatoa matibabu sahihi kwa mgonjwa na kumhakikishia usalama wake, hii pia itapunguza upotevu wa muda na fedha kwa kufanya ufuatiliaji wa matibabu sehemu nyingine ama kupewa dawa wakati hakuna ugonjwa. Kufanya ugezi kunachangia maendeleo katika Jamii " amesema Mahilla .
Kwa upande wake Bi. Clara Mwinami Afisa Vipimo TBS ametoa wito kwa Hospitali ambazo hazijafanya Ugezi wa Vifaa katika Maabara zao kufika TBS kwa maana Uhakiki wa Usahihi wa Vipimo wa Vifaa vyao utawasaidia kuaminika kwa Huduma wanazozitoa
