Breaking

Wednesday, 12 March 2025

PIC YAIPONGEZA TBA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI NZUGUNI DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),Mhe.Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12,2025 mara baada ya kamati yake kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),kwa ujenzi wa nyumba bora huku ikiwasisitiza kuendelea kusimamia matunzo ya nyumba hizo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 12,2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Augustine Vuma wakati kamati hiyo ilipotembelea awamu ya pili ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi 3500 unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Mhe.Vuma , amesema mradi huo umebuniwa kwa ubunifu wa hali ya juu na unatekelezwa kwa viwango vinavyoridhisha. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha nyumba hizo zinatunzwa vizuri ili zidumu kwa muda mrefu.

“Napongeza Wizara, TBA kwa ubunifu huu mzuri, hakikisheni zinasimamiwa vizuri ili kuwepo makazi ya kutosha kwa watumishi wa serikali na wateja hao waendelee kufurahia huduma za nyumba nzuri.

Aidha ameishauri TBA kushirikiana na taasisi kama TARURA ili kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya mradi huu kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wake Kaimu katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme,Mhandisi Mwanahamis Kitogo amesema kuwa wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na kamati ya PIC pamoja na ushauri waliowapatia ili kuboresha huduma wanazozitoa kwa jamii hasa katika utendaji na usimamizi wa nyumba wanazojenga.

“Maelekezo yametoka wakati kuna sera na miongozo ambayo tayari Wizara imeshaitoa kwa ajili ya kuboresha TBA katika utendaji wake wa kazi zaidi kwa hiyo maelekezo hayo tuliyoyapokea ni kama nyongeza ya jitihada ambazo tayari Wizara imeshazifanya kwa hiyo tutakwenda kutasimamia na tutafanya vizuri zaidi ya hapa tunavyofanya,” amesema Mhandisi Mwanahamisi

Naye Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro, amesema TBA itaingia ubia na sekta binafsi ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa haraka na kwa ufanisi. Amebainisha kuwa TBA tayari imesaini makubaliano na wawekezaji kutoka nje ambao watashiriki katika awamu ya pili ya mradi.

“Mbali na kushirikiana na sekta binafsi, tunapunguza gharama za ujenzi kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata zege hapa Nzuguni,” amesema Arch. Kondoro.

Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Meneja Mradi kutoka TBA, Emmanuel Julius almesema kuwa awamu ya pili ya uendelezaji inahusisha ujenzi wa nyumba 60 za chini na nyumba 90 zitakazokuwa kwnehe majengo matatu yenye sakafu 5 kila moja ili kuwa na matumizi sahihi ya ardhi na kufikia lengo kwa urahisi na ubora.

“Katika mpango wa utekelezaji wa awamu ya pili umeanza na ujenzi wa nyumba 50 za chini na maghorofa mawili ambayo kila moja lina uwezo wa kuchukua familia 30, unatekelezwa ba TBA kwa utaratibu wa Buni jenga kwa gharama ya sh. Bilioni 28.2.”

Katika nyumba 50 zilizoanza kujengwa katika awmau hii ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo nyumba 23 kazi ya kupaua inaendelea na nyumba 24 zipo hatua ya msingi, tatu zimekamilika ambapo moja itatumiwa kwa huduma za afya na moja kituo cha polisi.”

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakikagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),Mhe.Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12,2025 mara baada ya kamati yake kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme(DTES), Mhandisi Mwanahamisi Kitogo,akiipongeza Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa kufanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro,akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages