
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) na Afisa Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) wakisaini makubaliano ya mashirikiano Machi 7,2025 NM-AIST Tengeru Kampasi Jijini ArushaMakamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) wakisaini makubaliano ya mashirikiano Machi 7,2025 NM-AIST Tengeru Kampasi Jijini Arusha.
........
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Benki ya NMB wamesaini Mkataba wa hati ya mashirikiano unalolenga kutambua, kuhatamia na kuendeleza vipaji katika Teknolojia za kidigitali.
Makubaliano hayo ya miaka mitano, yamesainiwa Machi 7, 2025 katika taasisi hiyo, Kampasi ya Tengeru Jijini Arusha, ambapo NMB imewakilishwa Afisa Mkuu wa Rasirimali Watu, Emmanuel Akonaay.
Makamu Mkuu wa taasisi Prof. Maulilio Kipanyula akizungumza katika hafla hiyo, amesema kuwa, sehemu ya makubaliano ni pamoja na namna ambavyo taasisi hiyo itashirikiana na NMB katika kutafuta rasilimali fedha kwa pamoja, kwa ajili ya kuendeleza matokeo ya utafiti na bunifu zinazozalishwa na wanataaluma na wanafunzi ili kuweza kufikia jamii na viwanda.
Amesema kuwa, makubaliano hayo pia ni kuitumia Benki ya NMB kama sehemu ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kupeleka wanafunzi kwa ajili ya kupata uzoefu ili kujua kinachoendelea katika jamii.
"Eneo lingine ambalo tumekubaliana ni kuona namna ambavyo NMB na Nelson Mandelea wanavyoweza kuchagiza vijana wanaomaliza masomo yao kuweza kuajiriwa na kujiajiri, tutawapiga msasa ili wakitoka wawe na uelewa mpana kuhusu masuala ya ujasiriamali, kusudi wawe na uwezo wa kutumia maarifa hayo kuajiriwa kirahisi zaidi au kujiajiri wenyewe" Alisema Prof.Maulilio
Ameongeza kuwa, lengo la taasisi ya taaluma na NMB ni kuwa na mchango katika kuzalisha ajira mpya kupitia eneo la teknolojia, ambalo ni fursa ya kiubunifu katika kuzaa matunda yanayotarajiwa.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB, Bw. Emmanuel Akonaay amesema, makubaliano hayo yanalenga kukuza uwezo wa teknolojia na kuweka mustakabali chanya wa watanzania katika teknolojia kupitia taasisi hizo, kwa kuweka misingi imara kwenye ukuaji wa teknolojia nchini.
Ameeleza kuwa, NMB wanaamini maendeleo endelevu yanategemea zaidi uwezeshaji wa rasilimali watu katika maarifa na ujuzi stahiki ili kuweza kukabiliana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, ambapo Benki ya NMB imeahidi kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali kwa kubaini rasilimali watu wenye uwezo mkubwa katika eneo la teknolojia na mawasiliano.
Ameongeza kuwa, Benki hiyo inalenga kukuza na kuhimiza utamaduni, na kuja na teknolojia zinazo hamasisha ujasiriamali na utatuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya fedha, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kifedha ili kuweza kuwafanya wahitimu kuwa na uelewa mkubwa kuhusu masuala ya fedha na kuweza kufanya maamuzi sahihi kwenye nyanja mbalimbali.
Sambamba na hayo akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Nelson Mandela Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Mipango, Fedha na Utawala Prof. Suzana Augustino amesema, makubaliano hayo yameweka historia kwa taasisi hiyo ya kufikia viwanda na kuweka misingi katika kutekeleza makubaliano hayo na kugusa sekta ya tehama upande wa rasilimali fedha ambalo ni eneo lenye changamoto nchini.
Amebainisha kuwa, kwa makubaliano hayo kutakuwa na mabadiliko makubwa lengo likiwa ni kuhakikisha uchumi wa jamii katika nchi unakua na suala zima la tehama linawafikia watu wote walio mijini na vijijini hususani wanawake ambao ndiyo kundi kubwa linalosahaulika.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akiongea na ujumbe kutoka NMB walipomtembelea ofisini kwake leo Machi 7,2025 kwa ajili ya kusaini makubaliano ya mashirikiano.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) na Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) wakisaini makubaliano ya mashirikiano Machi 7,2025 NM-AIST Tengeru Kampasi Jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) akimkabidhi zawadi Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya mashirikiano Machi 7,2025 katika ukumbi mdogo wa mkutano katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya mashirikiano Machi 7,2025 katika ukumbi mdogo wa mkutano katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.

Mhadhiri Mwandamizi Dr. Devotha Nyambo ( kulia) akitoa maelezo kuhusu Komputa yenye uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa ( HPC) kwa wajumbe wa NMB walipotembelea Kituo cha Tehama Machi 7,2025.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay ( kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya hati mashirikiano Machi 7,2025 katika ukumbi mdogo wa mkutano katika Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.