Makamu Mwenyekiti wa kampeni ya Mama Asemewe, Verynancy Mrema akizungumza na wanahabari jijini Mwanza kuelekea kongamano la Binti wa Leo, Samia wa Kesho.
Mabinti wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini kupitia kampeni yao ya 'Mama Asemewe' wameandaa kongamano kubwa la 'Binti wa Leo, Samia wa Kesho', kwa lengo kutumia mifano ya mafanikio ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha mabinti kutimiza ndoto zao.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 08, 2025 katika ukumbi wa Bwalo la Jeshi uliopo Kona ya Nyegezi jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Makamu Mwenyekiti wa kampeni ya Mama Asemewe, Verynancy Mrema amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano wa kuingwa akiwa ni mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhfa huo mkubwa hivyo wao kama mabinti watahakikisha wanamuunga mkono.
Mrema amesema Dkt. Samia pia amekuwa chachu ya kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora kwa kujenga shule mpya katika mikoa yote nchini huku wakitoa pongezi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendelea kuamini uwezo wake na kumteua kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
"Kwa kipindi kifupi cha Rais Dkt. Samia madarakani, Serikali imejenga shule maalum za Sekondari za wasichana katika mikoa 26 nchini ili kuongeza wigo wa elimu kwa mtoto wa kike", amesema Mrema akibainisha kuwa hiyo ni miongoni mwa sababu za kumuunga mkono Rais Samia.
Hata hivyo Mrema amebainisha kuwa bado kuna changamoto zinazowakabili mabinti vyuoni ikiwemo ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, magonjwa ya zinaa, ndoa na mimba za mapema kabla ya wakati hivyo wanaomba Rais Dkt. Samia awasaidie kuanzisha taasisi itakayowasaidia mabinti wa vyuo na vyuo vikuu nchini ambapo wamependekeza taasisi hiyo iitiwe 'Binti wa Leo, Samia wa Kesho Foundation'.
Naye Katibu wa kampeni ya 'Mama Asemewe' Mkoa wa Mwanza, Marietha Mtawa amewahimiza mabinti wa vyuo na vyuo vikuu jijini Mwanza kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo litakalowasaidia kuhamasisha kupitia mifano ya mafanikio ya Rais Dkt. Samia.
Kwa upande wake Katibu Idara ya Vijana na Uhamasishaji kampeni ya Mama Asemewe, Furaha Panja amesema palipo na mafanikio ya mabinti, vijana pia hawakosi hivyo nao wajitokeze kwenye kongamano hilo na kuunga mkono juhudi zake za kuhamasisha mabinti kuwa viongozi wa kesho.
Na George Binagi- GB Pazzo, Mwanza
Makamu Mwenyekiti wa kampeni ya Mama Asemewe, Verynancy Mrema (katikati akizungumzia kongamano la Binti wa Leo, Samia wa Kesho linalotarajiwa kufanyika jijini Mwanza. Kulia ni Katibu wa Idara ya Mabinti na Uwezeshaji wa kampeni ya Mama Asemewe, Benedicta Oshoa na kushoto ni Katibu wa kampeni hiyo Mkoa wa Mwanza, Marietha Mtawa.
Makamu Mwenyekiti wa kampeni ya Mama Asemewe, Verynancy Mrema akizungumza na wanahabari jijini Mwanza kuelekea kongamano la Binti wa Leo, Samia wa Kesho.
Mabinti wa vyuo na vyuo vikuu nchini wakiwa tayari kwa kongamano la Binti wa Leo, Samia wa Kesho.
Mabinti wa vyuo na vyuo vikuu nchini wakiwa tayari kwa kongamano la Binti wa Leo, Samia wa Kesho.
Wanasema, 'Mama Mitano Tena'.
Wanasema, 'Mama Mitano Tena'.
Wanasema, 'Mama Mitano Tena'.
Katibu Idara ya Vijana na Uhamasishaji kampeni ya Mama Asemewe, Furaha Panja akihamasisha vijana jijini Mwanza kushiriki kongamano hilo.
Tazama video hapa chini

PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi