TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imesaini mkataba na Kampuni ya TIL Construction Limited kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma hivi karibuni.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema ujenzi huo ni sehemu ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo COSTECH wametengewa Shilingi bilioni 18 kwa ajili ya kuboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo hilo jipya.
Dkt. Nungu amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha menejimenti ya mifumo elimu ya juu katika kuwezesha mageuzi ya elimu kiuchumi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya COSTECH.
“Kwa hiyo tunafanya ukarabati hapa jengo la makao makuu Dar es Salaam, tumeshapata mkandarasi, tumeshapata vibali pia tunajenga jengo Dodoma,” amesema.
Amesema kiasi hicho cha fedha Sh. Bilioni 18, jumla ya Sh. Bilioni 8 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la STI Complex na ukarabati wa jengo lililopo.
"Ujenzi huu unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12, na baada ya hapo makao makuu ya COSTECH yatakuwa Dodoma, huku ofisi za Dar es Salaam na Zanzibar zikihifadhiwa kama ofisi za kanda". Amesema Dkt. Nungu.
Ameongeza kwa sasa wanafanya ukarabati wa jengo la makao makuu jijini Dar es Salaam..." tumeshaanza hatua zote muhimu, pamoja na ujenzi wa Dodoma, tutanunua vifaa vya kisasa ili kuimarisha mchango wetu katika mageuzi ya kiuchumi,” amesema Dkt. Nungu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL Construction Limited, Ding Fubing, ameeleza kuwa kampuni yake itajitahidi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL Construction Limited, Ding Fubing (kulia) wakionesha mikataba waliosaini kwaajili ya ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL Construction Limited, Ding Fubing (kulia) wakisaini mkataba wa ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL Construction Limited, Ding Fubing (kulia) wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (kushoto) akizungumza katika hafla ya utiaji saini na Kampuni ya TIL Construction Limited, kwaajili ya ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL Construction Limited, Ding Fubing akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI Complex) jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO