![](https://mzalendo.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA0018-860x501-1.jpg)
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma,kuhusu kuhitimisha msimu wa biashara ya bidhaa za kilimo kupitia mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa mwaka 2024/2025 na kujiandaa na msimu mpya wa 2025/26.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA0017-1024x607.jpg)
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari,leo Februari 7,2025 jijini Dodoma,kuhusu kuhitimisha msimu wa biashara ya bidhaa za kilimo kupitia mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa mwaka 2024/2025 na kujiandaa na msimu mpya wa 2025/26.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,amesema mfumo wa Stakabadhi za Ghala, umeendelea kuwa chombo muhimu katika kuimarisha urasimishaji wa biashara ya mazao kwa kuweka uwazi, kuongeza ushindani wa bei na kuwahakikishia wakulima masoko ya uhakika.
Dkt.Jafo,ameyasema hayo leo Februari 7,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari , kuhusu kuhitimisha msimu wa biashara ya bidhaa za kilimo kupitia mfumo huo kwa mwaka 2024/2025 na kujiandaa na msimu mpya wa 2025/26.
“Mfumo huu umeleta tija kubwa kwa wakulima wetu kwa kuhakikisha kuwa wanapata bei stahiki za mazao yao kwa wakati na bila vikwazo vya madalali wasio waaminifu. Aidha, urasimishaji huu unaongeza imani ya wanunuzi kutoka kutoka nje ya Tanzania,”amesema Jafo
Dkt.Jafo amesema katika kipindi hicho serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuchukua hatua za kuimaerisha mfumo huo.
Amesema kuwa, wadau hao ni pamoja na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Soko la Bidhaa Tanzania, TAMISEMI, Sekta Binafsi, Taasisi za Fedha pamoja na Mamlaka ya Biashara Tanzania.
“Tumeshuhudia ongezeko la mazao yanayouzwa kupitia mfumo huu, ongezeko la ghala zilizosajiliwa na ushiriki mkubwa wa wakulima katika kuuza mazao yao kwa utaratibu rasmi,”amesema Dkt.Jafo
Aidha, amesema katika msimu wa 2024/2025, jumla ya bidhaa 14 zilikusanywa na kuuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, zikiwemo Chai, Choroko, Dengu, Kahawa, Kakao, Korosho, Maharage, Mahindi, Mbaazi, Mchele, Mihogo, Mpunga, Soya, na Ufuta.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo huo, wameshuhudia ongezeko kubwa la uzalishaji na ukusanyaji wa mazao, ambapo jumla ya kilogramu 810,230,588 zilikusanywa, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na msimu wa 2023/2024, ambapo kilogramu 451,192,592 zilikusanywa.
Amesema kuwa ongezeko hilo halikuakisiwa tu katika kiwango cha mazao bali pia katika thamani ya mapato ya wakulima.
“Kutokana na wingi wa bidhaa pamoja na kuimarika kwa bei sokoni, wakulima walilipwa jumla ya Sh.Trilioni 2.9, ongezeko la asilimia 142 ikilinganishwa na Sh.Trilioni 1.2 walizopata msimu uliotangulia,”amesema
Waziri Jafo, amesema hali hiyo ni uthibitisho wa jinsi mfumo wa stakabadhi za ghala unavyoendelea kuwa chombo madhubuti cha kuhakikisha wakulima wananufaika ipasavyo na jasho lao.
Vile vile, amesema kuwa pamoja na faida kwa wakulima, ongezeko hili la thamani limezinufaisha pia halmashauri zilizoshiriki katika mfumo huo.
Amesema mapato yatokanayo na ushuru yameongezeka kutoka Sh.bilioni 36 msimu wa 2023/2024 hadi kufikia Sh. bilioni 87 msimu huu unaokamilika.
Aidha amesema kuwa hali hiyo ni ishara kuwa mfumo huo siyo tu unawanufaisha wakulima bali unachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya serikali za mitaa, na hivyo kusaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.