Breaking

Saturday, 8 February 2025

WATEKAJI WAWILI WALIOTEKA WANAFUNZI WAUAWA MWANZA,

 

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewaua watu wawili wanaouhusika na tukio la utekaji wa wanafunzi wawili,baada ya watu hao waliokuwa na mapanga kuanza kuwashambulia askari waliokuwa wakiwaokoa watoto hao katika eneo la nyegezi jijini mwanza wanafunzi waliotekwa February 5 mwaka huu katika mtaa wa Kapri Point wakati wanafunzi hao wakilekea shuleni.

Tukio hilo limetokea February 8 2025 katika mtaa wa Nyabulogoya kata ya Nyegezi jijini Mwanza ambapo kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishna wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema jeshi hilo baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuhusu uwepo wa Watoto hao katika moja ya nyumba iliyopo katika eneo hilo ndipo askari walipoizingira na kuamuru watekaji hao kufungua mlango,ambapo watekaji hao walijitokeza na wakiwa na mapanga na kuanza kuwashambulia askari hao ambao nao walijihami kwa kuanza kujihami kwa kuwafyatulia risasi watekaji ambao walipoteza Maisha.

Aidha kamanda Mutafungwa amesema jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wote wanaodaiwa kuhusika na utekaji wa watoto wao kwa namna yoyote ili kudhibiti tabia ya utekaji wa Watoto katika mkoa wa Mwanza

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo pamoja na mambo mengine wamepongeza hatua ya jeshi la polisi kuwaua watu hao na kuomba juhudi hizo kuendelea ili kuwadhibiti watu wenye tabia za utekaji ambazo zimekuwa zikijitokeza.

Alfajiri ya February 5 mwaka huu watu hao,mmoja wa watu hao alilisimamisha gari ya kubeba wanafunzi,ambapo baada ya muda mfupi mtu huyo alimkaba dereva shingoni na kisha kuwateka watoto hao na kutokomeo nao kusikojulikana
.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages