Breaking

Monday, 10 February 2025

WASIRA AMJULIA HALI GACHUMA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amemjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa (NEC), Ndugu Christopher Gachuma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando jijini Mwanza.

Ndugu Gachuma amelazwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari jana katika Kijiji cha Gesarya, Kata ya Lung'abure, wilayani Serengeti Mkoa wa Mara alipokuwa akielekea katika Ziara ya Makamu Mwenyekiti Wasira.

Majeruhi mwengine katika ajali hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ndugu Kemilembe Ruta pamoja na dereva wa gari hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, majeruhi wote wa ajali hiyo wanaendelea vizuri.

Ndg Wasira amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo kesho atahutubia mkutano mkubwa utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages