Kikundi cha ngoma ya kabila la Wafipa cha Mama Chanje wakionyesha Manjonjo yao ya kucheza ngoma zenye ujumbe mbalimbali mjini Sumbawanga, Rukwa, Tanzania hivi karibuni.
Kikundi cha ngoma ya kabila la Wafipa cha Mama Chanje wakionyesha Manjonjo yao ya kucheza ngoma zenye ujumbe mbalimbali mjini Sumbawanga, Rukwa, Tanzania hivi karibuni.
Na Mwandishi wetu, Sumbawanga, Rukwa
Wadau wa utamaduni wametoa wito kwa vikundi vya ngoma za utamaduni kusajili nyimbo zao kwenye Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ili kulinda hati miliki.
Hatua hiyo inalenga kuwasaidia kulipwa pale nyimbo zao zinapotumiwa na wasanii wakubwa ambao mara nyingi hupata fedha nyingi na kufaidika huku wahusika wakiambulia patupu.
Wito huo ulitolewa mjini Sumbawanga hivi karibuni wakati wa kikao kazi cha watunga sheria ndogo ndogo kilicholenga kujadili na kuja na mwongozo wa kutengeneza sheria ndogondogo Mkoani Rukwa zitakazosaidia kulinda na kukuza masuala yote ya urithi wa utamaduni usioshikika.
Akiongea katika kikao hicho, Afisa Michezo na Utamaduni wa Mkoa wa Rukwa bwana Adam Evarist alisema mara nyingi vikundi vya ngoma vimekuwa vikitunga nyimbo nyingi nzuri za lugha za asili bila kusajili na kusema kuwa iwapo watasajili, wataweza kukaa mezani na kutengeneza kipato kutokana na ubunifu wao.
“ Ni vema sheria ndogondogo zikajumuisha masuala ya utambuzi na tozo ili kuwezesha vikundi vya ngoma za asili kunufaika na kazi zao kuliko ilivyo sasa,” alisema Afisa huyo.
Kwa upande wake, mmoja wa machifu maarufu wa kabila la wafipa Chifu Kapele alisisitiza umuhimu wa kutengeneza Makumbusho ambazo zitaandika simulizi za wafipa kwenye kuta na kuzisajili na kuzirithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
“ Kumekuwepo na tabia ya waigiza filamu kutoka nje ya bara la Afrika kuja kuchukua simulizi za Afrika na kutengeneza filamu ambazo huingiza fedha nyingi huku Jamii husika ikishindwa kunufaika. Ni vema sheria ndogondogo zikalinda hati miliki ya simulizi na mali kale zote katika makabila yetu ili zisitumike kwa manufaa ya wengine tu bali Jamii husika iweze kufaidi,” alisisitiza Chifu Kapele.
Kikao kazi hicho kiliandaliwa na Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii ( TAMCODE) kwa ufadhili wa mradi wa UNESCO- Alwaleed Philanthropies wenye lengo la kutengeneza fursa za kiuchumi kwa vijana na wanawake na kutunza utajili wa urithi wa utamaduni nchini Tanzania