Timu ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo tarehe 11 Februari, 2025 imeendelea na zoezi la kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango katika eneo la Kilwa Masoko mkoani Lindi.
Zoezi hilo limeenda sambamba na Semina ya kodi kwa wafanyabiashara wa eneo hilo ambapo wamekumbushwa kufanya usajili pamoja na makadirio ya kodi ya mwaka 2025.
Aidha kwa upande wao wafanyabiashara wa Kilwa wameishukuru TRA kwa kufanya semina hiyo pamoja na kuwatembelea kwa ajili ya kuwapa elimu ya kodi na kuomba zoezi hilo liwe endelevu kwani kila siku kuna wafanyabiashara wapya wanaoingia kwenye biashara.