BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) wameziomba Mamlaka za serikali za mitaa katika ngazi zote kuchukua hatua stahiki kupambana na watu wanaotupa taka ngumu katika mifumo ya maji pamoja mifumo hiyo ya maji kuwa safi na kuimarisha njia na mikondo ya maji iwe safi wakati wote.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa NEMC,Dkt Immaculate S Semesi,wakati akizungumza na waandishi kuhusu taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya hali hewa nchini(TMA)iliyotolewa hivi karibuni kuhusu uwepo wa mvua kubwa .
Dkt Semesi amesema kwa kuzingatia sheria ya mazingira na Usimamizi wa maafa sura 242 ambayo inayowataka Mamlaka ya Serikali za mitaa kufuatilia usimamizi wa mazingira na majanga kwa karibu maeneo ya uchimbaji wa madini na vifusi ili kuhakikisha jamii husika inakuwa salama na majanga yanayoweza kujitokeza maeneo yao.
"Tunatoa wito kwa serikali za mitaa kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za Serikali na wadak wa Mazingira na Jamii kwa Ujumla kuhakikisha Miundombinu ya kupitisha maji safi na taka iko sawa ,kutoa elimu kwa wananchi katika kuhifadhi mazingira,Uvunaji wa maji yamvua pamoja na ujenzi unaozingatia jiografia ya eneo husika"amesema
Hata hivyo,Dkt Semesi amesema ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha wanaweka mazingira safi na salama ili kuepusha mafuriko na mlipuko wa magonjwa ambayo yamekuwa yakirudisha nyuma jitihada za ujenzi wa Taifa.
"Baraza tunawatadharisha wananchi kujiepusha kwa namna yeyote ile kwenye kuchangia uharibu wa mazingira kwa kuzingatia kadhaa ikiwemo kufuatili taarifa za TMA ili kuwa na tahadhari maeneo yenye viashiria hatarishi"Amesema Dkt Semesi.
Dkt Semesi amesema kwa miaka hivi karibuni mataifa kadhaa yamekumbwa na majanga mbalimbali yanayosababishwa na athari za shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia ya nchiBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira(NEMC) wameziomba Mamlaka za serikali za mitaa katika ngazi zote kuchukua hatua stahiki kupambana na watu wanaotupa taka ngumu katika mifumo ya maji pamoja mifumo hiyo ya maji kuwa safi na kuimarisha njia na mikondo ya maji iwe safi wakati wote.