Breaking

Tuesday, 11 February 2025

Naibu Waziri Asema Serikali Ya Tanzania Inaendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

Februari 10, 2025 Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), amebainisha kuwa Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kufanya mabadiliko makubwa katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Mhe. Nyongo aliyasema hayo Februari 11, 2025, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua Kongamano la nne la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia.

Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kurekebisha sheria za biashara, kufuta ada, tozo, na faini ambazo hapo awali zilikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara.

Katika hotuba yake, Mhe. Nyongo aliwahamasisha wawekezaji kutoka Italia kuwekeza nchini Tanzania akisisitiza kuwa ni mahali sahihi kwa uwekezaji barani Afrika.

Aidha, katika kongamano hilo, Mhe. Nyongo alishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (Memorandum of Understanding) kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Muhimbili na Chuo Kikuu cha Rome, ikilenga kuimarisha utafiti na afya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages