Breaking

Tuesday, 11 February 2025

MZUMBE YAKABIDHI VIFAA VYA KUTENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI KWA TAASISI ZA LEVO NA MORO PARALEGAL CETRE

Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Maudhui mafupi ya KITEHAMA hii leo umekabidhi vifaa vyenye thamani ya takriban Milioni Thelathini kwa taasisi ya Legal Vision Organisation (LEVO) ya Lushoto - Tanga) na Morogoro Paralegal Centre (MPLC -Morogoro) katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Lushoto, Mkoani Tanga.

Akikabidhi vifaa hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo Kikuu Mzumbe kama yalivyoainishwa kwenye Mpango mkakati wa Chuo, yaani Kufundisha, kufanya tafiti zenye tije, na kutoa ushauri wa kitaalamu.

“Mradi huu unajumuisha dhamira ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa maono na dhamira yake ya kushughulikia mahitaji muhimu ya jamii, hususani suala la elimu ya kisheria kwa umma na upatikanaji wa haki hasa kwa makundi yenye uhitaji zaidi, wakiwemo watu wenye hali ngumu ya kiuchumi, wanawake, watoto na walemavu, ambao hawawezi kumudu gharama za uwakilishi wa mawakili binafsi” Amesitiza Prof. Mwegoha.

Amesema Mradi wa Kuimarisha Utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria unalenga kuziba pengo kwa kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria katika kutoa elimu ya kisheria itakayowafikia watu wengi zaidi kiurahisi bila gharama, kwa kushirikiana na Kliniki ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu Mzumbe, na mashirika mengine ya wasaidizi wa kisheria kupitia maudhui yaliyoundwa kitehema.

Awali Mratibu wa Mradi Bw. Edgar Rutatora amesema wasaidizi wa kisheria wana jukumu muhimu katika kutoa suluhisho la kivitendo la kuimarisha upatikanaji wa haki, kutoa ushauri wa kimsingi wa kisheria, elimu ya kisheria, kuwezesha upatanishi na utatuzi mbadala wa migogoro, kutetea haki za binadamu, na kutoa uhamasishaji wa jamii kuhusu sheria, hasa haki na wajibu wa raia kikatiba na sheria za nchi.

“Kwa kuwapatia wasaidizi wa kisheria uwezo wa kutengeneza maudhui ya kitehama, tunawawezesha kuwafikia watu wengi zaidi na ufanisi mkubwa zaidi. Chuo Kikuu Mzumbe kinatambua umuhimu wa ushirikiano katika kufikia malengo yake. Hivyo, mradi huu unafanya kazi kwa karibu na wasaidizi wa kisheria katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.” Amesisitiza Bw. Rutatora

Hakimu Mkazi wa wilaya ya Lushoto Mhe. Rose Ngoka amesema taasisi ya LEVO wilayani Lushoto imekuwa na msaada mkubwa katika kutatua migogoro kwa njia ya amani.

Katika Wilaya ya Lushoto maudhui ya mtandaoni yamesambazwa katika Mabasi, Shule za Sekondari, Hospitali na Vituo vya Afya, Kumbi za starehe na kambi za elimu.

Mradi wa Kuimarisha Utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia maudhui mafupi kwa Matumizi ya Tehama ni sehemu ya Mradi wa VLIR-UOS ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo kikuu Mzumbe na Chuo kikuu cha Ghent cha nchini Ubelgiji.
Mgeni rasmi wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akikabidhi vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya LEVO (legal vision organisation)
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya lushoto baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni kwa Taasisi zisizo za kiserikali (LEVO na Morogoro Paralegal Centre)
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni kwa taasisi zisizo za kiserikali (LEVO na Morogoro Paralegal Centre)
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha huduma za utoaji wa msaada wa kisheria kwa maudhui mafupi - VLIROUS Bw. Edger Rutatola akielezea kuhusu lengo la hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni kwa taasisi ziziso za kiserikali (LEVO na Morogoro Paralegal Centre) na namna vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha shughuli mbalimbali katika taasisi hizo
Mgeni rasmi wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akifungua rasmi hafla hiyo na kushukuru jitihada zote zilizofanyika kufanikisha makabidhiano ya vifaa
Mgeni rasmi wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akikabidhi vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Morogoro Paralegal Centre
Mgeni rasmi wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni  ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla hiyo
Mgeni rasmi wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kutengeneza maudhui mtandaoni ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William mwegoha (kulia) akikabidhiwa zawadi na waratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya LEVO (legal vision organisation)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages