Breaking

Friday, 31 January 2025

WMA YAHIMIZA WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA UJENZI KUZINGATIA MATAKWA YA VIPIMO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKALA wa Vipimo (WMA) amewataka wafanyabiashara wa bidhaa za ujenzi nchini kuhakikisha bidhaa wanazouza zinakidhi matakwa ya sheria ya vipimo kwa lengo la kusaidia kuepusha hasara kwa watumiaji wa mwisho.

Agizo hilo amelitoa leo January 31,2025 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Vipimo Ilala Muhono Nashon wakati wa kufanya zoezi la ukaguzi wa bidhaa za ujenzi katika maduka ya Buguruni.

Aidha Nashon amesema kuwa wamekagua nondo, simenti, mabati pamoja na bidhaa nyingine zinazohusiana na masuala ya ujenzi.

Amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu kwani litafanyikia mara kwa mara kwa sababu bidhaa hizo,zinaingia kwa wingi sokoni ambapo itawalazimu kukagua kila wakati.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa Sheria ya Wakala wa Vipimo inapomkuta mtu nakosa kuna adhabu zinatolewa ikiambatana na mahakamani kwa mtuhumiwa kutokana na hujuma hiyo.

"Sheria ya Wakala wa Vipimo adhabu yake ya chini kabisa ni shilingi laki moja na kiwango cha juu kinafikia Milioni 20 au kifungo Cha miaka miwili"Amesema

Pamoja na hayo Muhono ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa za ujenzi,kupitia matakwa ya Sheria za Vipimo kwa umakini ili wajikite kuzingatia vipimo bila kufanya udanganyifu.

"Mzalishaji, kama unazalisha nondo mm16 kweli iwe mm16, kama unazalisha bati ni geji 30 kweli iwe geji 30".Amesema Nashon.

Vilevile amesema kuwa kwa wananchi wanaohitaji kutoa taarifa kuhusiana na suala la Vipimo kufika katika ofisi zao za Mikoa au kupiga simu bure nambari 08000110097.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages