Breaking

Thursday, 30 January 2025

MADIWANI WA MANISPAA YA SHINYANGA WAPITISHA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI MWAKA WA FEDHA 2025/2026.. BILIONI 40.2 KUTUMIKA

  

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamepitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo jumla ya shilingi 40,271,905,280/= zinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali na zitatumika katika shughuli za utoaji huduma, utawala, na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mapendekezo haya ya Shilingi Bilioni 40.2 yamewasilishwa katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo, Januari 30, 2025.

Katika mkutano huo, madiwani wamekubaliana na bajeti hiyo huku wakitoa ushauri wa kuboresha baadhi ya maeneo, hasa kuhusu huduma ya maji safi na salama na ujenzi wa barabara, kutokana na hali mbaya ya miundombinu ya barabara katika maeneo mengi.

Akitoa taarifa kuhusu Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Manispaa ya Shinyanga, Mensaria Mrema, amesema kuwa fedha zitakazokusanywa zinatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato, ikiwa ni pamoja na Vyanzo vya mapato ya ndani Shilingi 6,403,000,000/= na Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu Shilingi 6,497,592,000/=

Vyanzo vingine ni Ruzuku ya matumizi mengineyo: Shilingi 1,357,940,000/=, Ruzuku ya mishahara: Shilingi 22,219,049,200/= na Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Wahisani: Shilingi 3,794,324,080/=.
Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Manispaa ya Shinyanga, Mensaria Mrema.

Aidha, Mrema ameeleza kuwa katika utekelezaji wa mpango wa mwaka 2024/2025, Halmashauri ilikusanya jumla ya shilingi 3,465,718,440.18/-, sawa na asilimia 54% ya makadirio ya mapato ya ndani.

"Mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilipanga kukusanya shilingi 38,053,453,654/= ambapo kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai 2024 hadi Desemba 2024) imeweza kukusanya jumla ya shilingi 3,465,718,440.18/- sawa na asilimia 54% ya makadirio yote yanayotokana na vyanzo vya ndani",amesema Mrema.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko, amesisitiza kuwa mapendekezo hayo ni hatua ya mwanzo na madiwani bado wanaruhusiwa kutoa maoni kwa ajili ya marekebisho zaidi.

Ameshauri kuboreshwa kwa mifumo ya ukusanyaji mapato kwa kutumia busara, kuepuka kutumia nguvu na badala yake wazingatie sheria na taratibu.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, ameipongeza Halmashauri kwa maendeleo inayoyafanya katika ukusanyaji mapato na ameshauri elimu zaidi itolewe kwa wananchi kuhusu ulipaji kodi na ushuru, ili waweze kulipa kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Revocatus Lutunda, ameahidi kutekeleza ushauri na maelekezo yaliyotolewa na viongozi katika mkutano huo.

Ajenda kuu za kikao hicho zilijumuisha kupitia mapitio ya mpango wa bajeti ya mwaka 2023/2024, nusu ya mwaka wa fedha 2024/2025, mapendekezo ya mapato ya ndani kwa mwaka 2025/2026 na mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza Januari 30,2025 wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Revocatus Lutunda akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Revocatus Lutunda akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Manispaa ya Shinyanga, Mensaria Mrema akitoa taarifa kuhusu Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages