Breaking

Tuesday, 14 January 2025

DKT. NDIEGE AAGIZA VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA NA SACCOS KUWATUMIA WAKAGUZI WA NDANI



Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege akizungumza kwenye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC uliofanyika leo Januari 14,2025 jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege ameagiza Vyama Vikuu vya Ushirika na SACCOS kubwa nchini kuajiri na kuwatumia ipasavyo Wakaguzi wa ndani ili kuongeza ufanisi wa vyama hivyo.

Dkt. Ndiege ameyasema hayo leo Januari 14, 2025 Jijini Dodoma wakati akizindua Kamati ya Ukaguzi ya TCDC ambapo amesema Wakaguzi ni watendaji muhimu wanaohitajika kusaidia kubaini changamoto za kwenye ushirika na kushauri namna ya kukabiliana nazo ili kuendelea kuwa na usimamizi imara wa Sekta ya Ushirika.

“Serikali imedhamiria kuimarisha ushirika kwa maslahi mapana ya nchi, Tume hii ni chombo muhimu na kinaangaliwa kwa jicho la pekee kwa maslahi makubwa ya nchi yetu, hivi sasa tuna takribani vyama vya ushirika 7,000 na vilivyosajiliwa kwenye Mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika ni 6,500 baadae tutatoa takwimu kama vipo ambavyo havifanyi kazi,”amesema.

Aidha, amesema serikali ya awamu ya sita imeipa uzito sekta ya ushirika na kwamba Tume hiyo ni chombo muhimu kwa serikali na mfumo pekee utakaowasaidia watanzania ni ushirika ili kuwa na nguvu ya pamoja ambapo takriban watu milioni nane wanajihusisha na vyama vya ushirika.

Dkt.Ndiege amesema ni lazima Tume ambayo ni msimamizi wa sekta ya ushirika kuwa imara na wajumbe wa kamati hiyo walioteuliwa wameingia kwa sifa na uwezo wao wa kufanya kazi ili kusaidia usimamizi wa Vyama vya Ushirika.

Awali, Mwenyekiti Mstaafu wa Kamati hiyo, CPA Evance Assenga amesema kamati yake ilishauri na kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya rasilimali, uwazi na uwajibikaji wa Tume ili kuleta ufanisi kwenye sekta hiyo, huku akiishauri kamati mpya kutumia kwa umakini taarifa za Mkaguzi wa Ndani kwa kuwa zitawasaidia kwenye ukaguzi.

Naye, Mwenyekiti wa Mpya wa kamati hiyo, CPA Elihuruma Lema ameahidi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na weledi mkubwa ili kuongeza tija kwenye sekta ya ushirika nchini ambayo ina idadi kubwa ya watu wanaochangia uchumi wa nchi.



Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege akizungumza kwenye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC leo Januari 14,2025 jijini Dodoma.



Mwenyekiti wa Mpya wa kamati ya ukaguzi ya TCDC, CPA Elihuruma Lema akizungumza kwenye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC leo Januari 14,2025.


Mwenyekiti Mstaafu wa Kamati yaUkaguziyaTCDC, CPA Evance Assenga akizungumza kwenye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC leo Januari 14,2025.


Mkaguzi Mkuu wa ndani Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Mwanaidi Kalela akizungumza kweye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC leo Januari 14,2025 Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, (kushoto) akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC, CPA Elihuruma Lema, katika Uzinduzi wa Kamati hiyo.

Picha ya pamoja ya washiriki kwenye uzinduzi wa Kamati ya Ukaguzi ya TCDC leo Januari 14,2025.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages