Breaking

Sunday, 8 December 2024

WIZARA YAFUNGA MWAKA KWA KUZINDUA TUZO ZA KITAIFA ZA UTALII NA UHIFADHI



Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali kwa mara ya kwanza katika historia Desemba 20, mwaka huu inakwenda kuzindua tuzo za sekta ya Utalii na Uhifadhi.

Akuzungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Dkt. Abbasi amesema Wizara imeamua kufanya hiyo ili kutoa hamasa kwa wadau wa sekta hizo waweze kufanya vizuri hivyo kuchangia kwenye uchumi wa taifa.

Amefafanua kuwa ujumla ya tuzo 11 za heshima zitatolewa kwa wadau mbalimbali kutambua mchango wao katika sekta hizo.


Aidha, ameongeza kuwaTanzania imeendelea kufanya vizuri katika kupokea watalii wa kimataifa na kuvunja rekodi zilizowekwa kabla ya kipindi cha UVIKO – 19 mwaka 2019.

"Kwa mujibu wa Ripoti ya Nusu Mwaka ya Takwimu za Utalii ya Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism Barometer report) katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Julai, 2024, Tanzania imeshika nafasi ya kwanza Afrika kwa nchi zilizotembelewa na idadi kubwa ya watalii." Amefafanua Dkt. Abbasi

Aidha, amesema tukio la uzinduzi wa tuzo hizo utaambatana na burudani mbalimbali za wasanii.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages