WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameiagiza Bodi ya Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha linasimamia vyema shirika hilo na kuhakikisha liendeshwa kibiashara.
Maagizo hayo ameyatoa leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Mhe. Silaa amemtaka Mwenyekiti wa Bodi hiyo David Nchimbi kutengeneza mpango utakalitoa Shirika lilipo na kulipeleka kwenye uendeshaji kibiashara ikiwa ni kutekeleza maagizonya Rais Samia,
"Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza shirika kuhakikisha linaendeshwa kibiashara hivyo Mwenyekiti atengeneze mpango utakaotutoa tulipo na kupeleka shirika kwenye uendeshaji kibiashara " amesema Mhe. Silaa.
Aidha Mhe. Silaa amesema serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya mawasiliano ya Taifa ikiwemo mkongo wa taifa ambao umeunganisha karibu nchi nzima na kuna miradi mbalimbali na kuna kuna miradi mikubwa ya mawasiliano mradi wa ktuo cha Taifa cha data hivyo ni nia ya Rais Samia kuona uwekezaji huo mkubwa uliofanywa kwa fedha za wananchi uweze kuleta tija kwa kujiendesha kibiashara na kuiona ile thamani ya fedha iliyotolewa.
Amesema iwapo Shirika likiendeshwa vyema linaweza kukuza sekta mbalimbali na kuleta mapinduzi makubwa ikwenye uchumi wa nchi.
"Hivyo Mwenyekiti na wajumbe tekelezani hayo na ninawaahidi milango ya wizara iko wazi, na mtambue uendeshaji wa shirika uko chini ya bodi hivyo uwajibikaji uko chini ya mabega yenu siimamieni menejimenti vizuri ili tufike tuendako" amesema,
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo Nchimbi ameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kuwa na shirika jipya na kulipeleka mbele zaidi na kwa kasi.
Amesema wajumbe wana uwezo mkubwa na wamesikia maelekezo yaliyotolewa na watayafanyia kazi na hakuna litakalowashinda .