Breaking

Saturday, 7 December 2024

WANACHAMA WA SDC SACCOS LIMITED WAFANYA MKUTANO MKUU WA 22,... WAKABIDHIWA HATI SAFI


Chama cha Akiba na Mikopo cha Shinyanga District Council Limited SACCOS kimefanya mkutano mkuu wa 22 wa mwaka 2024 kujadili na kupokea agenda mbalimbali za chama hicho.

Mkutano huo umefanyika leo Jumamosi Disemba 07, 2024 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ukihudhuriwa na viongozi na wanachama wa chama SDC SACCOS LTD.


Akisoma taarifa ya chama cha Shinyanga District Council Limited SACCOS kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho Epafras Mazina Makamu Mwenyekiti Aisha Omary ameeleza mipango, maendeleo, mafanikiao na ukuaji wa chama kwa ujumla.


"Hadi kufikia Septemba 2024 jumla ya mtaji wa chama ulikuwa unafikia zaidi ya milioni 200, chama kimeendelea kufanya shughuli zake ambazo ni kutunza akiba, kutumza hisa na faida, kutoa mikopo ya muda mrefu mfupi kwa wananchama wake, bodi ya SDC SACCOS itaendelea na mpango wa kuboresha na kuleta faida kwa njia ya kubunj huduma mbalimbali zenye manufaa kwa wanachama bila kutumia gharama kubwa kwa kuzingatia athari na kuwezesha kununua hisa za SCULLT zenye thamani ya Milioni 300 ili kufikia hisa ya Milioni 500", amesema Aisha Omary.


Awali akisoma taarifa ya kamati ya usimamizi wa chama hicho kuanzia Januari 01 hadi Septemba 30, katibu Ndugu Festo Stanslaus amesema idadi ya wanachama wa SDC SACCOS LTD kwa sasa imefikia 202 huku ongezeko la Tsh 87,250,000/= kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2024.


Mwenyekiti wa chama cha akiba na mikopo Shinyanga District Council Limited SACCOS Epafras Mazina amesema chama hicho kimekuwa mkombozi kwa watumishi wa umma kwa kuondokana na mikopo yenye liba kubwa kwenye makampuni ya kifedha na kujiunga na chama hicho cha akiba na mikopo chenye liba nafuu.


Kwa upande wake mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Deogratias Momburi ametoa elimu juu ya masuala ya hisa na umuhimu wa uwekaji wa akiba na kwenye chama cha SDC SACCOS LTD na kuwakumbusha wanachama wajibu wa wanachama kwenye chama ikiwemo kufuata na kutekeleza sheria ya vyama vya ushirika, masharti ya chama na kukubaliana na maazimio ya chama pamoja na chama kutumizi mifumo ya kidigitali.


Naye mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga David Rwazo ametoa rai kuchukuliwa hatua kwa wanachama wasiorejesha mikopo kwa wakati kichukuliwa hatua na kuwataka wanachama wa SDC SACCOS kuhamasisha watumishi wengine kujiunga na chama hicho kwa manufaa ya chama na maisha yao.


"Kama uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga tumeendelea kukiunga mkono cha Akiba na Mikopo SDC SACCOS LIMITED na kuendelea kuwa msaada mkubwa kwa watumishi wetu, ningependa nishauri jambo juu ya urejeshwaji wa mikopo ya dhararu kwa wakati inayotolewa kwa wanachama kuwa watakaoshindwa kurejesha kwa wakati ni vyema kuwachukulia hatua stahiki", amesema David Rwazo.


"Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ina jumla ya watumishi 2437 ukiangalia wanachama wa SDC SACCOS LIMITED ni 202 mpaka sasa hivyo ni wasihi kama wanachama wa akiba na mikopo SDC SACCOS LIMITED",


"Tuendelee kuhamashisha watumishi wengine kutoka halmashauri ua Shinyanga waweze kujiunga na chama hiki ili kuepukana na mikopo ya kausha damu huko mitaani lakini pia ni lazima kama chama kuwa na watu wa masoko ili kuvutia wanachama wengine na kuvuka wastani wa watu 4 kwa mwaka kwa maslahi mapana ya chama chetu", ameongea David Rwazo.


Aidha Rwazo amekipongeza chama hicho kwa kupokea hati safi kutoka kwa kutoka kwa mkaguzi wa nje kwenye ripoti inayohusu taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 31/12/2023.

Makamu Mwenyekiti Aisha Omary akisoma taarifa ya chama hicho kwa niaba ya  Mwenyekiti wakati wa mkutano huo.

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Deogratias Momburi akizungumza wakati wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa chama cha Shinyanga District Council Limited SACCOS Epafras Mazina akizungumza wakati wa mkutano huo.

Katibu wa chama cha Shinyanga District Council Limited SACCOS Festo Stanslaus akizungumza kwenye mkutano huo.

Mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga David Rwazo akizungumza wakati wa mkutano wa mkuu wa 22 wa chama cha Akiba na Mikopo cha Shinyanga District Council Limited SACCOS.

Mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Shinyanga David Rwazo akizungumza wakati wa mkutano wa mkuu wa 22 wa chama cha Akiba na Mikopo cha Shinyanga District Council Limited SACCOS.

Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

Mwenyekiti wa mkutano mkuu wa 22 wa Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited) Moshi Walioba akizungumza wakati wa mkutano huo.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages