Breaking

Thursday, 12 December 2024

TANZANIA NA BENKI YA DUNIA WASAINI MIKATABA MIWILI YA DOLA MILIONI 104 KUKUZA USAWA WA KIJINSIA KUPITIA MRADI WA PAMOJA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”.

Mikataba hiyo imejumuisha mkataba wa dola za Marekani milioni 4 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9.5 ni msaada na Mkataba wa dola za Marekani milioni 100 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 238 ni mkopo wenye masharti nafuu.

Akizungumza leo Desemba 12, 2024 katika hafla hiyo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mradi wa PAMOJA utasaidia kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar. 

Amesema hilo litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wanawake kupitia mifumo rasmi ya kifedha na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia". Amesema 

Aidha amesema kuwa Mradi huo utawanufaisha wanawake wapatao 319,850 moja kwa moja na walengwa wengine 399,000 wakiwemo wajumbe wa kaya za wanufaika.

"Kukuza usawa wa kijinsia si suala la wanawake peke yao, ni msingi wa taifa la kidemokrasia, lenye haki, na linalostawi. Kuondoa tofauti za kijinsia kunaboresha uzalishaji na kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi".

"Kwa wanawake na wasichana wa Tanzania, naahidi jitihada na dhamira yetu kamili pamoja tuvunje vikwazo vinavyozuia maendeleo na kupanda mbegu za usawa ili kila Mtanzania bila kujali jinsia yake apate fursa ya kustawi kwa kadri ya uwezo wake". Ameeleza Dkt. Nchimbi.

Pamoja na hayo Dkt. Nchemba amehimiza ukamilishaji kwa wakati wa masharti yote ya awali (conditions of effectiveness) kuwezesha kuanza rasmi kwa mradi ya miradi hiyo miwili. 

Amesema Kukamilika kwa masharti hayo kutasaidia utekelezaji wa miradi kuanza kwa wakati na kuepusha ucheleweshaji, uwezekano wa kuomba nyongeza ya muda pamoja na kupunguza gharama za mkopo (commitment fees) ambazo huanza kutozwa baada ya mwaka wanne wa utekelezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete wanatarajia mradi huo utaanza kutekelezwa mapema na kuona matokeo ya utekelezaji pamoja na faida watakazozipata walengwa wa mradi huo.

Amesema mradi huo utatatua changamoto za kijinsia za kijamii na kiuchumi kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi na kubainisha mila potofu ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima mradi huo umekusudia kujenga nyumba salama 10 kwa ajili ya kuwahifadhi Watoto wanaokumbana na ukatili wa kijinsia pamoja na kujenga vituo 200 vya malezi salama na makuzi ambapo vituo 184 vitakuwa Tanzania Bara na 16 vitajengwa Zanziber.

“Afisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii wamekuwa wakihangaika kupata ofisi za kufanyiakazi na kutoa huduma pamoja na vifaa kazi ikiwemo usafiri, sasa  kwa kutumia fedha hizi watapata Ofisi 40 za maafisa Maendeleo ya Jamii na Ofisi 40 za Maafisa Ustawi wa Jamii”, Amesema Dkt. Gwajima. 

Pamoja na hayo amepongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali anazofanya kuwainua wanawake kiuchumi ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi wa PAMOJA.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete wakisaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza mara baada ya kusaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete akizungumza mara baada ya kusaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza mara baada ya kusaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakipata picha ya pamoja viongozi wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia mara baada ya kusaini mikataba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104 sawa na takribani shilingi bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA” leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages