Breaking

Wednesday, 11 December 2024

Mahafali ya 17 DUCE : Dkt. Jakaya Kikwete Asisitiza Umuhimu wa Utafiti DUCE

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MKUU wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kuongeza juhudi katika nyanja za utafiti ili kiweze kupata heshima kimataifa.

Amesema ingawa chuo kinakutana na changamoto za majengo, maabara, na vifaa, bado ni muhimu kuendelea na juhudi za kuboresha utafiti na elimu.

Ameyasema hayo leo 11, 2024 kwenye Mahafali ya 17, Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema Chuo kimeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuanza kwa ujenzi wa majengo mapya chini ya Mradi wa HEET ambapo ukikamilika utaboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Aidha amesema Chuo kimeendelea kufanya vizuri katika nyanja za utafiti, ubadilishanaji maarifa, menejimenti ya rasilimali watu, huduma za jamii na miundombinu.

Amesema katika mahafali za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa mwaka 2024, jumla ya wahitimu 9,493 wamehitimu masomo yao ambapo wanawake ni asilimia 47.6 ya wahitimu wote.

Pamoja na hayo Prof. Anangisye amesema Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu muhimu na kutoa fedha za uendeshaji wa Chuo kwa ujumla.

“Serikali imeendelea kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya Juu wakiwemo wanafunzi wa DUCE”. Amesema Prof. Anangisye.

Nae Rasi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam, Prof. Stephen Maluka amesema kupitia Mradi wa HEET, Chuo kimepata zaidi ya shilingi bilioni kumi kwaajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu na majengo ya Chuo, kujenga majengo mawili ya ghorofa na miundombinu mingine mipya vikiwemo viwanja jumuishi vya michezo.

Amesema kuwa mpaka sasa mkandarasi ameshapatikana na ameshaanza kazi ya ujenzi na ukarabati.

“Inatarajiwa kuwa kufikia mwaka ujao majengo haya yatakuwa yameanza kutumika na kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia”. Amesema 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages