Breaking

Thursday, 12 December 2024

BODI YA WAKURUGENZI TBS YATEMBELEA MIPAKA YA TUNDUMA NA KASUMULU

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Othman Chande Othman imefanya ziara ya kutembelea ofisi za TBS zilizopo katika mipaka ya Tunduma na Kasumulu ili kujionea shughuli zinazofanyika.

Dhumuni la Ziara hiyo ni kuona changamoto zilizopo na kuzitafutia mkakati na kuielekeza Menejimenti ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwezesha biashara.

Aidha Bodi hiyo imefanya ziara hiyo Desemba 10 katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe na Desemba 11 kwenye mpaka wa Kasumulu mkoani Mbeya.

Pamoja na hayo Bodi imeielekeza menejimenti ya TBS kuja na mikakati ya bidhaa zinazoingia kupitia njia za panya na kukwepa ukaguzi ikiwa ni pamoja na  kuendelea kutoa elimu ya madhara ya kutumia bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake na TBS.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages