Breaking

Wednesday, 13 November 2024

TALAKA YASABABISHA AJALI,WATU 35 WAFARIKI, YAJERUHI 43



Watu 35 wamefariki na wengine 43 kujeruhiwa, baada ya mwanamume mwenye umri wa miaka 62 aliyetambuliwa kwa jina la Fan, kuwagonga na gari huko Zhuhai, kusini mwa China.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Fan, aliyepatikana akiwa amejeruhiwa kwenye gari lake, alitenda uovu jumatatu Novemba 11 kutokana na kuchanganyikiwa na mgawanyiko wa mali katika talaka yake ya hivi majuzi, kulingana na ripoti ya abcNEWS.
Kulingana na NPR, mamia ya wafanyakazi wa uokoaji kutoka mkoa wa Zhuhai na Guangdong walijibu, pamoja na wafanyakazi zaidi ya 300 wa afya kutoka hospitali tano wakifanya kazi bila kuchoka kuwahudumia waathiriwa.

Rais wa China Xi Jinping alizungumzi tukio hilo katika taarifa Jumanne jioni, Novemba 12, akitaka mhusika aadhibiwe vikali kwa mujibu wa sheria.

Alizitaka serikali za mitaa kuzidisha hatua za kuzuia ili kushughulikia hatari zinazoweza kutokea, kuzuia matukio makubwa, na kudhibiti migogoro mara moja.

Wakati uo huo, mkasa huu ulitokea wakati Zhuhai alipokuwa mwenyeji wa maonyesho ya anga ya Jeshi la Ukombozi la Watu, ambayo yalifunguliwa siku hiyo hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages