Breaking

Wednesday, 20 November 2024

MOROGORO WATAKA EWURA ISIMAMIE HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI ZIPATIKANE



Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa Mkutano huo.

........

Wadau mbalimbali wa mkoa wa Morogoro wametoa maoni, ushauri na kuwasilisha malalamiko yao kuhusu huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na EWURA Kanda ya Kati, leo tar 20.11.24.

Mkutano huo uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa, ulilenga kupokea maoni na kutathimi hali ya utoaji huduma zinazodhibitiwa na EWURA mkoani hapo ambapo aliwataka wadau hao kutoa maoni na malalamiko bila woga, ili kuisaidia EWURA kuendelea kuboresha huduma za nishati na maji.

“Tuisaidie EWURA kuwasimamia watoa huduma, tutoe maoni yetu kwa ufasaha, uwazi na bila woga, ili huduma hizi za nishati na maji ziboreshwe kwa ustawi wetu”, alieleza.

Dkt. Musa pia, ameisihi EWURA, kuisimamia kwa karibu Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Morogoro (MORUWASA), ili watoe huduma bora na fanisi kwani kumekuwapo malalamiko juu ya kukosekana kwa huduma ya maji mara kwa mara.

Wadau walioshiriki mkutano huo ni kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Manispaa, wamachinga, walimu, wajasiriamali, wafanya biashara, viongozi wa dini, madereva bajaji na bodaboda. Wengine ni watu wenye ulemavu, watoto, wazee, jukwaa la wanawake, EWURA CCC, MORUWASA na TANESCO.

Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Mha. Hawa Lweno, alisisitiza kuwa, malalamiko na maoni yaliyopokelewa yatafanyiwa kazi kwa wakati ili watumia huduma za nishati na maji mkoani hapo wafurahie huduma bora.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa Mkutano huo.



Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Bi. Hawa Lweno, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.



Baadhi ya Wadau wa Mkoa wa Morogoro wakitoa maoni yao kuhusu sekta zinazodhibitiwa.
Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Musa Ally Musa, katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau kutoka katika makundi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Mha. Hawa Lweno, kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Kati, Bw. Juma Singano.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages