Breaking

Wednesday, 6 November 2024

MAKATIBU WAKUU WA BIASHARA WA AFRIKA WATAKIWA KUTEKELEZA AFCFTA KWA VITENDO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs),akizungumza na washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Na.Mwandishi Wetu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs) ametoa rai kwa Makatibu Wakuu hao kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) na kuiwezesha Afrika kujitegemea, kuwa na maamuzi na sauti ya pamoja yenye nguvu ili punguza madhara ya misukosuko ya uchumi wa dunia na kuleta maendeleo kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni barani humo.

Dkt. Abdallah ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024.

Akiipongeza Jamhuri ya Liberia kwa kuridhia Mkataba wa AFCFTA, amezihimiza nchi nyingine ambazo bado hazijaridhia Mkataba huo kukamilisha mapema taratibu za ndani za uridhiwaji ili kuwa na utekelezaji wa pamoja wa Mkataba wa AfCFTA unaochochea maendeleo ya sekta mbalimbali kama viwanda, biashara, miundombinu na kukuza uchumi ndani ya Afrika.

Aidha, Dkt. Abdallah amefafanua kuwa Mkutano huo utapokea Taarifa kutoka kwa Kamati za Biashara Mtandao, Uwekezaji, Biashara ya Bidhaa, Wanawake na Vijana katika AfCFTA, Haki Bunifu na Biashara ya Huduma ili kuzijadili na kuziwasilisha katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Biashara Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 - 10/11/2024

Naye Waziri wa Biashara na Mtangamano wa Kikanda wa Ethiopia, Mhe.Yasmin Wohabrebbi, amesema AFCFTA ni nguzo imara inayolenga kuongeza kasi ya biashara baina ya nchi za Afrika, kuimarisha nafasi ya biashara ya Afrika katika soko la dunia, na kuinua mamilioni ya watu kutoka umaskini kwa kuwa unaunganisha watu bilioni 1.3 katika nchi 55 zenye Pato la Taifa la dola trilioni 3.4 za Marekani.

Akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo amesema lengo kubwa ni kuhakikisha Watanzania wanashiriki katika kuzalisha bidhaa bora zitakazopata soko hilo la Afrika ili kukuza biashara, kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika(STOs) akiongoza Mkutano huo Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/202

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo pamoja na Wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) wakiongozwa na Mshauri Mkuu wa AFCFTA Dkt.Tsotetsi Makong, Novemba 05, 2024 akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha maandalizi kabla ya kushiriki Mkutano wa 19 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STOs) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/2024.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs),akizungumza na washiriki wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu (STOs) kutoka Nchi Wanachama wa AFCFTA unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Majadiliano katika Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (STOs)Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Mwenyekiti wa Mkutano wa 19 wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika(STOs) akiongoza Mkutano huo Novemba 05, 2024. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Novemba 5 – 7, 2024 ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AFCFTA kwa mwaka 2024 kuanzia Januari – Disemba 2024. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika kuanzia tarehe 01 – 03/11/2024 na utafuatiwa na ngazi ya Mawaziri utafanyika tarehe 8 - 10/11/202
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages