Breaking

Tuesday, 26 November 2024

HIZI NDIYO CHANGAMOTO ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

     



John Francis Haule

UTANGULIZI 

Mtangamano na ushirikiano wa nchi zinazounda Jiografia ya Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda ulianza hapo kale hasa miaka ya 1926 kipindi cha utawala wa Mjerumani wakati huo ikifahamika kama East Africa Province.

 Na baada ya utawala wa kikoloni kuondolewa na mataifa haya kuwa huru  kisiasa waasisi wa wakati huo waliunda jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967 na ilipofika 1977 jumuiya hiyo ikasambaratika  na sababu kuu inaelezwa kuwa ni kutoelewana kati ya Iddi Amini Sada Rais wa Uganda na Julius Nyerere Rais wa Tanzania na kutofautiana kiiitikadi na ideolojia baina ya nchi washirika.

Jumuiya hii ya awali ilidumu kwa kipindi cha miaka kumi tu  japo ilikuwa na madhumuni mazuri na yenye mantiki ya kimajumuiya (Pan Africanism Objectives.)

Mnamo mwaka 1999  Viongozi wa mataifa haya matatu waliamua kuhuisha jumuiya hii kwa kuandaa  mkataba au katiba(EAC TREATY)  na huu mkataba ulianza kutumika rasmi mwaka 2000 hivy huu mwaka utakuwa ni mwaka wa 25 yaani jubilee ya miaka 25 ya jumuiya hii ya Africa mashariki tangu kuhuishwa kwa jumuiya hii ya Afrka Mashariki.

Mpaka sasa jumuiya hii ina wanachama  8 yaani wana chama 5  zaidi wamejiunga na jumuiya hii ya Afrika Mashariki wana chama hawa ni Burundi,Rwanda, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Sudan Kusini na Somalia. Huu ni uthibitisho tosha kuwa kuendeleea kwa nchi kuvutiwa kujiunga na EAC inadhihirisha kuwa hii jumuuiya iko madhubuti na imara katika madhumuni yake.

SIFA NA VIGEZO VYA NCHI  KUJIUNGA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI  ( EAC MEMBERSHIP)

Ili nchi yoyote iweze kuwa na vigezo vya kukubaliwa kujiunga na jumuiya ya EAC  ni lazima iwe na sifa zifuatazo.

Kigezo cha utawala bora ndani ya nchi (good governace)

Utawala wa sheria (rule of law)

Kuthamini haki za binadamu (observation of human rights)

Haki za kijamii (social justice)

Mshabihiano wa sera za kiuchumi na za kijami  sawia na zile za jumuiya(social and economic policies being compartible with those of community)

Mkabala wa kijiografia,(geographical proximity)

Demokrasia yani uhuru wa watu,uchaguzi n.k

Ifahamike kuwa moja kati ya madhumuni makuu ya EAC ni kuunda dola la kisiasa la pamoja yaani Political federation au co.federation

Na ili kufikia kwa hilo dhumuni la mtangamano wa hizi  nchi zinatakiwa kufuata hatua zifuatazo:

HATUA ZA KUUNDA SHIRIKISHO HIZI HAPA  

               ( PILARS OF EAC)

Ushuru wa forodha (customs unions)

Soko la pamoja (Comon market)

Sarafu ya pamoja (monentary union)

Shirikisho  la kisiasa au mtangamano wa kisiasa(political federation or co.federation)

TAASISI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC ORGANS)

Jumuiya ya Afrika Mashariki ina fanya kazi kupitia taasisi zake

Baraza la mawaziri (the council) hili lina undwa na mawaziri wa mambo ya nnje na ushirikiano wa Afrika Mashariki toka nchi  wanachama

Mahakama ya haki za binadamu (EA Court of justice)

Hii ina husika na utoaji haki hasa kwa  mashitaka ambayo mahaka za ndani ya nchi washirika wasipo rizika hupeleka rufani  kwa mahaka ya haki za binadamu ya Afrika mashariki

 Bunge la Afrika Mashariki(EALA) muhimili huu ni kutunga sheria za Afrika Mashariki ikiwemo bajeti ya jumuiya.

 Sekretariet au kamati tendaji hii inaundwa na makatibu wakuu wanaoteuliwa na wakuu wa nchi mwanachama


 MADHUMUNI  YA JUMUIYA YA AFRIkA MASHARIKI

Kwa ujmla madhumuni ya jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni haya.

Utatuzi wa migogoro  miongoni mwa nchi wanachama( peace making and Conflict resolution) hili ni dhumuni muhimu sana katika dhima ya uundwaji wa mtangamano huu wa Afrika mashariki. Mfano mwaka 2008  mgogoro wa kisiasa nchini Kenya  ulitatuliwa na  jumuiya hii kupitia mwenyekit wake Rais Jakaya kikwete. Na kupelekea nchi ya Kenya kuwa na Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka mitano.

Na hivi sasa tumeona nchi Wanachama wamepeleka jeshi huko DRC Congo ili kuondoa kundi la M23 hii yote ni kuhakikisha nchi wanachama wanakuwa salama ndani ya jumuiya.

Kukuza soko la pamoja na kupanua wigo wa biashara miongoni mwa nchi mwanachama. Tukirejea kwa misingi ya mtangamano huu msingi wake moja wapo ni soko la pamoja yaani common market kwa kuja pamoja hizi nchi nane zimepanua wigo wa soko kwa idadi ya watu takribani milioni miata.hili ni soko kubwa lina saidia kushajihisha biashara na kukuza wigo wa uwekezaji. 

Mfano Kiwanda cha kuzalisha mbolea kilichopo Dodoma eneo la Nala ENTRACOM FERTILIZER kilichowekezwa na mwekezaji toka Burundi. Hali kadhalika Bank ya CRDB imefungua tawi huko Rwanda n.k haya ni matokeo chanya ya uwepo wa huu mtangamano.

Kupambana na maradhi na mlipuko wa  magonjwa kwa pamoja. Kwa hili mwaka 2008 hadi 2009 wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa bonde la ufa (Rift valley fever) nchi zote zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki zilishikamana kuhakikisha ugonjwa huo una tokomezwa.

Kukuza diplomasia hususani ile ya uchumi miongoni mwa nchi wanachama (to consolidate diplomatic ties among the member states)

Kupambana dhidi ya ugaidi  (terrorism threat) kwa kuzingatia kuwa uharifu hauna mipaka,hivyo kupitia jumuiya majeshi ya hizi nchi hukutana na kubadilishana uzoefu wa kupambana na ugaidi na matishio mengine hususani  katika kanda ya bahari na vikundi vingine vinavyo weza hatarisha usalama wa  nchi wana chama na hata raia mfano Mngiki huko Kenya,M23 Huko DRC kongo. 

Kushajihisha uhuru wa raia  miongoni mwa nchi wanachama  ( to enhance freemovement of people  among the member states) na hili ni dhumuni kubwa na la msingi ime pelekea kuwa na hati moja ya kusafiria( E PASSPORT) miongoni mwa nchi wana chama na hata mipaka ya hizi nchi kwa wananchi wanchi wana chama kume punguza urasimu wa mipakana na hili lime chagiza ukuaji wa biashara  miongoni mwa nchi wana chama. Mfano hapa Arusha wafanaya biashara wengi wana peleka  bidhaa Kenya na hali kadhalika wakenya wana leta bidhaa hapa Arusha.

MAFANIKIO YA EAC

Mbali na changamoto ambazo zinazikabili hii jumuiya tangu kuhuishwa  mapa sasa imefanikiwa kwa mambo mengi.  Haya ni baadhi tu ya mafanikio 

 Uhuru  wa kusafiri miongoni mwa nchi wanachama. Hii imekuwa faida mtambuka kwa wananchi wa nchi  zote kuingia na kutoka katika nchi mwanachama uraismu huu umeondolewa na uwepo wa huu mtangamano wa EAC.

Imepunguza  changamoto ya Ajira hasa kwa kuwa na soko jumuishi, mfano walimu wa lugha ya Kiswahili na wale wa masomo ya sayansi wana pata ajira katika nchi wanachama.

Kuongezeka kwa wanachama  kutoka wale wa tatu wa awali mpaka nane.hili nifanikio kubwa na lakupongezwa na imedhihirisha kuwa hii jumuiya kwa sasa inamvuto kwa utendaji wake wa kazi na namna inavyo saidia kuimarisha umoja na mshikamano wa nchi mwanachama.

Imeshajihisha kukua kwa uwekezaji wa ndani, nahii ime dhihirika kwa nchi wana chama kuwa na uwezo wa kuwekeza  na kuanzisha miradi ya kiuchumi naya kijamii mfano uwepo wa chuo kikuu cha kimataifa cha kampala hapa Tanzania(Kampala Internatina University) 

Imefanikwa kutatua migogoro yenye mnasaba wa siasa,mfano  2008 klKenya baada ya uchaguzi, pia mgogoro wa Sudan na hata DRC Congo,  pia imepunguza  tishio la kiusalama wa kikanda hasa kutokana na juhudi za pamoja za kutokomeza makundi ya kigaidi na uasi mfano M23 na kundi la Mungiki  na intarahamwe makundi haya yamedhoofu kwa jitihada zinazo fanywa na jumuiya ya Afrika Mashariki


HIZI NI BAADHI YA CHANGAMOTO ZA JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI  (challenge facing E.A.C)

Ni muhimu kufahamu kuwa jumuiya hii inajiendesha kwa kujitegemea  na ikijiegeza katika michango inayo tokana na wanachama wake. Changamoto sio udhaifu bali ni kudhihirisha tu kuwa iko inatimiza majukumu yake vema. Hizi ni baadhi tu ya changamoto zake.

 Changamoto za kibajeti na michango. Kwenye hili nchi wanachama husuasua kutoa michango yake ya kueendeshea jumuiya hili linapunguza ufanisi wa jumuiya.

Kutozingatiwa kwa mkataba na itifaki zake (treaty and protocals) hasa swala la ujirani mwema na kuishi kwa Amani  hasa mataifa yaliyojiunga  hivi karibuni mfano DRC CONGO na RWANDA wakituhumiana kuhusu kundi la M23.

Utekelezwaji hafifu wa itifaki hasa soko la pamoja (common market) 

Lugha ya pamoja.haya mataifa kiasili bado yana lugha za watawala wa kikoloni hivyo kuna kuwa na change moto ya ma wasiliano baina ya nchi mfano Kiswahili TZ na nchi nyingine zina lugha za asili na za kikoloni.

Taasisi zake kuto fahamika majukumu yake kwa wananchi walio wengi. Mfano bunge la EALA vikao vyake havionekani mubashara kama ilivyo mabunge ya nchi wanachama.

MAONI NA MASWALI TUNAYO PASWA KUJIULIZA SISI WANA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI 

1.JE? Kuundwa kwa shirikisho la kisisas la Afrika mashariki lina wezekana kwa hata miaka 50 ijayo?

2 JE?  Kuna ulazima wa kuwa na shirikisho la kisiasa ?

3.JE?  wananchi wanaiona jumuiya ya Afrika mashariki kama ya kwao au bado wana hisia kuwa ni ya viongozi wa kisiasa zaidi kuliko wanachi?

4.JE? kwani ni lazima ardhi iwe sehemu ya shirikisho?

Maoni

Nimuhimu kujifunza katika historia hasa kwa  iliyo kuwa soviet ya zamani(USSR) ilivyo sambaratika mwanzoni mwa miaka 90

Hii ilitoa funzo kunapo kuwepo kwa shirikisho ni vizuri kukawa na nchi chache zilizofungamana vizuri kuliko kuwa na nchi nyingi ambazo hazioneshi ari ya kujidhatiti na misingi ya jumuiya.

Pia kuelekea shirikisho hususani sasa tukielekea kwenye kujadili sheria za sarafu ya pamoja (monentary union) ni muhimu tukawa na utaratibu mzuri ambao hautoathiri sarafu yetu.

KWA KUHITIMISHA

Jumuiya ya Afrika Mashariki ina uzuri wake hasa katika kukuza uchumi,uwekezaji na diplomasia ya kisiasa na kiuchumi kwa sasa nadhani tujikite kwenye haya yenye manufaa kwa wananchi.


Makala hii ,imeandikwa na

JOHN FRANCIS HAULE

MKUU WA SOKO KUU   LA ARUSHA

SIMU 0756717987 au 0711993907

Mail.haulej46@yahoo.com


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages