Breaking

Monday, 4 November 2024

Elimu ya Usalama Kuhusu Kemikali ya Sianidi Yazinduliwa Dar es Salaam

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Usafirishaji wa Kemikali ya Taifa, Transport and Logistic Limited, kwa kushirikiana na Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania, Mainline Carriers, na Swala Solution Limited, imezindua zoezi la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya kemikali ya sianidi (Sodium Cyanide) na hatari ya kuyasogelea magari yanayobeba kemikali hiyo.

Akizungumza leo Novemba 4,2024 wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Derick Masako amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali chini ya mamlaka ya GCLA bado wanaendelea kuwasisitiza wananchi kutosogelea magari yanayobeba kemikali ikiwemo ya sianidi pindi yanapopata ajali.

Amesema Kemikali hii ikimwagika na kuchanganyika na maji inaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu kwani inatoa hewa chafu ya sumu ambayo mtu akiivuta inaweza kumsababishia madhara makubwa na hata kupelekea kifo.

“Sianidi inatumika katika kuchenjulia,tunajua dhahabu ina thamani lakini upatikanaje wake unatumia kemikali mbalimbali,kemikali hii ina uwezo wakulainisha dhahabu ukiiweka inapotea kama sukari  ukiiweka kwenye maji,kwa hiyo ni kali sana,”amesema Mkemia Masako.

Kwa upande wake Meneja wa Afya ,Usalama na Mazingira wa kampuni ya Freight Forwaded Sadiki Yusufu amesema  kemikali hiyo ambayo ni bora kwa uchimbaji wa madini duniani ina madhara makubwa endapo ikiamwagika na kuingia maji.

“Kemikali ya sodiamu sianidi pamoja na kutumika katika masuala mengine yakimaabara nchini lakini asilimia 90 ya kemikali inatumika katika kuchimba madini,kemikali ina uwezo mkubwa wakulainisha dhahabu,ili ifike migodini uwa inasafirishwa". Amesema 

Aidha amesema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwaelimisha wananchi hasa wanaotumia vyombo vya usafirishaji wasigusane na hayo magari maana endapo gari litaanguka na kumwagika na  ikashika maji inaweza kuleta madhara kwa binadamu.

Amesema kemikali hiyo ambayo imeingia Tanzania mwanzoni mwa miaka 1990 inaweza kuondoa dhahabu kutoka kwenye mwamba kwa ubora zaidi kushinda mercury ambayo inasifika muda mrefu kwa kufanya shughuli hizo.

Amesema tangu iingie nchini imekuwa ikitumika kwa uangalifu na kwamba haijawahi kusababisha ajali ya aina yoyote iliyogharimu maisha ya watu.

Naye Ofisa Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Taifa Transport and Logistic Limited, Bestina Kitinya amesema hatua ya kwanza ya kujikinga na kemikali hiyo pindi ikimwagika barabarani basi watu watakaokuwepo eneo hilo watapaswa kuvaa barakoa na kukimbia umbali wa mita 100.

“Na unapokimbia hakikisha unakimbia kwa kuangalia upepo unapotokea, pia ikitokea mtu amemgusa yule ambaye ameathirika na kemikali hiyo ya Sianidi mfano dereva aliyekuwa akiendesha gari bila kujikinga anaweza kupata madhara pia, hivyo unapaswa kutomgusa sehemu zenye jasho,” amesema

Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Derick Masako akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu kemikali ya sianidi iliyofanyika leo Novemba 4,2024 Mbezi Stendi Jijini Dar es Salaam.
Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Derick Masako akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu kemikali ya sianidi iliyofanyika leo Novemba 4,2024 Mbezi Stendi Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Usalama, Afya na Mazingira kutoka Kampuni ya usafirishaji ya Freight Forwarders Tanzania, Sadiki Yusufu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu kemikali ya sianidi iliyofanyika leo Novemba 4,2024 Mbezi Stendi Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Taifa Transport and Logistic Limited, Bestina Kitinya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu kemikali ya sianidi iliyofanyika leo Novemba 4,2024 Mbezi Stendi Jijini Dar es Salaam.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages