Breaking

Tuesday, 5 November 2024

CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akielezea malengo ya Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Wa kwanza kushoto) akimsikiliza mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Vincent Ngure wakati akielezea mifumo ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya utumishi wa umma wakati wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said akisalimiana na Makamu wa Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) Bw. James Wasagami (Wa kwanza kulia) wakati alipowasili kushiriki kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 9 wa mtandao huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Wa pili kutoka kulia ni Rais wa Mtandao huo (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi na wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.



Mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Theresia Ngassa (kushoto) akigawa kablasha na kitambulisho kwa mmoja wa washiriki wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Prof. Patrice Lumumba ambaye ni Msemaji Mkuu wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman.



Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kutoa huduma kwa washiriki wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).



Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia usajili wa mshiriki wa Mkutano 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).



Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli wakati wa Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Na. Veronica Mwafisi-Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewaasa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) kuwa wabunifu katika kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuondokana na changamoto mbalimbali za watumishi wa umma na kukuza sekta hiyo kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo makubwa katika Bara la Afrika.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

“Mkutano huu wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu umefanyika katika kipindi ambacho dunia ina changamoto mbalimbali hivyo niwaase mtumie fursa ya mijadala mtakayoiendesha na mawazo mtakayoyatoa kupitia maazimio na mapendekezo yalete mtazamo chanya katika kutoa majawabu yatakayosaidia kukuza sekta ya umma kiuchumi na kijamii.” Amesema Mhe. Simbachawene

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, kupitia kaulimbiu ya mkutano huo inaonyesha ni kwa namna gani rasilimaliwatu katika utumishi wa umma ni nyenzo muhimu na ya thamani kubwa katika kila nchi ambapo Serikali huitumia kuwafikia wananchi wake katika kutoa huduma za kijamii na kiuchumi ili kukuza ustawi wa jamii husika.

Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza wawezeshaji wa Mkutano huo kwa mada mbalimbali walizozitoa kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo ambazo kwa asilimia kubwa zitasaidia kuleta mabadiliko katika utendaji kazi kupitia rasilimaliwatu zilizopo katika Bara la Afrika.

Kwa upande wake, Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, amesema kuwa katika mkutano huo wa 9 wajumbe watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa lengo la kuwezesha nchi za Bara la Afrika kupiga hatua za kimaendeleo kwa kutumia mbinu za kisasa.

“Mtandao huu umeanzishwa kwa lengo la kujenga uwezo wa rasilimaliwatu yenye matokeo chanya katika kuhudumia wananchi Barani Afrika hivyo kupitia Mkutano huu tutapata fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu ili kuzisaidia nchi zetu kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa mataifa.” Bw. Daudi amesema.

Mkutano huo wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia leo tarehe 4 hadi 7 Novemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Kaulimbiu ya Mkutano huo ni ‘Utawala Stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu’.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages