Breaking

Sunday, 10 November 2024

AFRIKA YATAKIWA KUTOKUWA NA MATABAKA KATIKA KUTEKELEZA AFCFTA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) unaofanyika Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.

......


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa nchi wanachama wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) kushirikiana kwa sauti moja yenye nguvu bila kujenga matabaka ya aina yeyote katika kutekeleza Mkataba huo ambao utaiwezesha Afrika kujitegemea na kuleta maendeleo Kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni kwa manufaa ya Bara la Afrika na wananchi wake.

Vilevile, Ametoa wito kwa Nchi hizo kuhakikisha zinatekeleza kwa vitendo yale yote waliokubaliana katika Mkataba wa AfCFTA na kwa kuweza kujitegemea ndani ya Afrika ili kupunguza madhara ya misukosuko ya uchumi wa dunia kama mabadiliko ya tabia nchi na madhara ya janga la UVIKO-19, na kuendelea kuweka mikakati imara kwa katika kuifikia Afrika tunayo itaka katika masuala ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Waziri Jafo amayesema hayo Novemba 9, 2024 akiwa kama Mwenyekiti wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) wa wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Mikutano ya AfCFTA kwa mwaka 2024. Aidha, Waziri jafo ameeleza jinsi Tanzania inavyochukua hatua mbalimbali katika kutatua changamoto za ufanyaji biashara chini ya AfCFTA kama kujenga Reli ya Kisasa ya SGR inayounganisha Bandari ya Dar es salaam na nchi jirani, Ujenzi wa Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) wa Megawati 2115 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya umeme viwandani na shughuli za kibiashara, ujenzi wa viwanja vya ndege, miundombinu ya barabara.

Ameendelea kufafanua hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa bandari za Dar es salaam, Tanga, na Mtwara, uimarishaji wa mifumo ya kidigitali pamoja na urekebishaji wa Sera ya Biashara mwaka 2003 kuwa na toleo la 2023 inayolenga kuongeza fursa za ushiriki katika biashara kwa sekta binafsi hususani wanawake na vijana.

Pia amebainisha kuwa amesema biashara baina ya nchi za Afrika kwa kutumia taratibu na vigezo vya AfCFTA imeanza kuongezeka ambapo Tanzania, imetoa jumla ya Vyeti vya Uasili wa bidhaa vipatazo 131 kwa Makampuni

Naye Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Taye Atske Selassie amesisitiza kuwa AfCFTA ni zaidi ya mkataba wa biashara; ni chombo chenye nguvu kitakachosukuma ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika, kuongeza biashara, ajira, na kupunguza umasikini, kuimarisha usalama wa chakula, kukuza usawa wa kijinsia, na kuharakisha utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika

Vilevile, Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene amesisitiza Nchi Wanachama kuendelea kuboresha sera, kurahisisha ufanyaji biashara, kukuza ushirikiano imara kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuendelea kujenga mustakabali wenye mafanikio kwa wananchi wote ikiwemo kukuza Biashara, kuendesha wa Mfumo wa Malipo na Makubaliano ya Kanda Huru ya Afrika (PAPSS), kuzindua wa Mfuko wa Marekebisho wa AfCFTA na kuendeleza Jukwaa la Biashara Afrika.

Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Katibu Mtendaji wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene katika ofisi za Umoja wa Afrika(AU) Jiji Addis Ababa, Ethiopia

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene kabla ya kushiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa pamoja na viongozi wengine wakisalimiana na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Taye Atske Selassie kabla ya hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) unaofanyika Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Ethiopia Mhe. Taye Atske Selassie pamoja na pamoja na Mawaziri wenzake wa Biashara pamoja na Makatibu Wakuu wa Biashara kabla ya hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) unaofanyika Novemba 9, 2024, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages