Breaking

Thursday, 31 October 2024

ZOEZI LA KUBADILISHA NOTI ZA ZAMANI KUANZA JANUARI 6, 2025

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema zoezi la kubadilisha noti za zamani litaanza rasmi Januari 6, mwakani na kwa kipindi cha miezi mitatu hadi Aprili 5, hivyo basi Watanzania wametakiwa kuziwasilisha fedha hizo benki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Sarafu BoT, Ilulu Ilulu amesema zoezi la ubadilishwaji litafanyika ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara nchini kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kilichowasilishwa.

Aidha amewataka Watanzania wahakikishe wanakwenda kubadilisha noti tu zilizo halali zenye alama za usalama na faida ya kufanya hivyo ni kupata thamani ambayo walidhani imepotea na baada ya miezi hiyo kupita watazifuta kabisa.

“Inapotokea kusitisha uhalali wa noti fulani wananchi hupewa muda maalumu wa kuzibadilisha noti hizo kabla ya kusitisha uhalali huo , hupewa fursa ya kubadilisha noti husika kwa kupewa kiwango kilekile". Amesema

Pamoja na hayo amewataka Watanzania kuacha kuuza na kukununua noti chakavu mitaani kwani ni kosa kisheria na kinachofanyika ni utapeli.

Amesema wananchi wanatakiwa kwenda kubadilisha noti hizo katika Benki za Biashara nchini kwani kuna madirisha maalumu ya kubadilishia fedha hizo.

“Suala la kununua na kuuza sarafu halipo kisheria ni kosa kwa sababu kinachofanyika hapo ni kumtapeli mwenzako kutokana na kutokuwa na taarifa, BoT imetoa fursa kwa Benk izote za Biashara nchini kuwa na dirisha la kubadilisha noti chakavu,”alisema.

Kutokana na hilo amewataka wananchi kwenda wenyewe kubadilisha fedha hizo katika madirisha yaliyofunguliwa katika benki zote za biashara kunufaika na huduma hiyo.

Noti za zamani ambazo zinatakiwa kuondolewa kwenye mzunguko ni shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.
Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Sarafu BoT, Ilulu Ilulu akionesha fedha ambazo zinatumika kwasasa pamoja na fedha za zamani ambazo zinahitajika kuondolewa kwenye mzunguko, alipokutana na waandishi wa habari leo Oktoba 31, 2024 kutoa taarifa ya mpango wa kuondoa noti za zamani  katika mzunguko wa sarafu.

Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Sarafu BoT, Ilulu Ilulu akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mpango wa kuondoa noti za zamani  katika mzunguko wa sarafu leo Oktoba 31, 2024 Jijini Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Sarafu BoT, Ilulu Ilulu akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mpango wa kuondoa noti za zamani  katika mzunguko wa sarafu leo Oktoba 31, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages