Breaking

Thursday, 31 October 2024

WAZIRI JAFO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA COMESA NCHINI BURUNDI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo leo tarehe 31 Oktoba 2024 amemuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Soko Huru la Kusina na mashariki mwa Africa(COMESA).

Mkutano huo umefanyika katika Jiji la Bujumbura nchini Burundi ukilenga kuimarisha Mtengamano wa kikanda kupitia kuongeza thamani kwa kilimo himilivu kwa mabadiliko ya Tabianchi na thamani ya Madini,na kuimarisha Utalii.

Tanzania inashiriki mkutano huo kama waangalizi kwani Tanzania bado ipo katika Mchakato wa kikamilisha utatu wa EAC-SADC-COMESA.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo ni moja na kuongeza fursa ya nchi ya Tanzania katika masuala ya biashara na kujenga uchumi wa nchi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages