Na: Mwandishi Wetu - Juba, Sudan ya Kusini
WAJASIRIAMALI kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania wamemshukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kushiriki maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Juba, Sudan ya Kusini.
Wakizungumza Wajasiriamali hao kwa nyakati tofauti wamesema uratibu uliofanywa na Serikali kugharamia usafiri wao na mizigo, hali hiyo imewapa chachu ya kushiri kwa wingi katika maonesho hayo.
Vile vile, Wajasiriamali hao watumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi wa Sudan ya kusini pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutembelea banda la Tanzania ili kujionea bidhaa bora zinazozalishwa na Watanzania.
“Sisi wajasiriamali tunafarijika sana na tunamshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutuwezesha kufika Sudan ya kusini ili tuweze kutangaza biashara zetu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Janeth Makundi
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Amos Nyandwi amesema Serikali imeendelea kuratibu ushiriki wa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati katika maonesho hayo ili waweze kutangaza biashara zao nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Jumuiya ya Afrika Mashariki (CISO Tanzania), Josephat Rweyemamu amesema maonesho ya Nguvu Kazi au Jua Kali yanalenga kutoa fursa kwa wajasiriamali kuonesha huduma na bidhaa wanazozalisha, kubadilisha uzoefu, ujuzi na taarifa na wajasiriamali wenzao katika Jumuiya sambamba na kukuza wigo wa masoko mapya.
Maonesho hayo yanaongozwa na kauli mbiu “Kukuza Ubunifu wa Kipekee na Maendeleo ya Ujuzi miongoni mwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki,”.
Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Pili wa Sudan ya Kusini, Mhe. Dkt. James Wani Igga ambapo maonesho hayo yamevutia Wajasiriamali zaidi ya 1,700 kutoka nchi zote Nane (8) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushiriki.
Sehemu ya wajasiriamali wa Tanzania wakiwa na Wateja waliotembelea banda la Tanzania kweye maonesho 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazu au Jua kali yanayoendelea katika viwanja vya Freedom Hall jijini Juba, Sudan ya Kusini.
Sehemu ya wajasiriamali wa Tanzania wakiwa na Wateja waliotembelea banda la Tanzania kweye maonesho 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazu au Jua kali yanayoendelea katika viwanja vya Freedom Hall jijini Juba, Sudan ya Kusini.