Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akimkaribisha Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) aweze kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akiwaongoza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuimba wimbo wa mshikamano daima wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakichangia mada wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliofanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Baraza la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya ya kufungua mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.