Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya Mtandao kwa watu wenye mahitaji maalum Mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uelewa wa pamoja namna ya kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni.
Mafunzo hayo yametolewa leo Alhamisi Oktoba 17,2024 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum amesemaTCRA inatekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watumiaji wote wa mitandao wakiwemo watu wenye ulemavu wanapata huduma salama na sahihi mtandaoni ikiwa ni utekelezaji wa Kampeni Kabambe ya 'Ni Rahisi Sana' yenye lengo la kuwahimiza watanzania wote wajilinde dhidi ya uhalifu mtandaoni.
Amesema Kampeni ya Ni Rahisi Sana imelenga kuwahimiza watanzania wote wajilinde dhidi ya uhalifu mtandaoni akieleza kuwa uwepo wa mazingira salama mtandaoni yatawezesha kufikia malengo ya uchumi wa Kidijiti.
“TCRA inatoa elimu kuhusu usalama wa mtandaoni kupitia kampeni za uhamasishaji kwa umma ikiwemo hii Kampeni ya Ni Rahisi Sana. Kampeni hii inahusisha jinsi ya kutambua uhalifu mtandaoni, uonevu wa mtandaoni na matapeli. Tunatoa mafunzo juu ya kutumia nywila salama, kujilinda dhidi ya utapeli wa kifedha mtandaoni na jinsi ya kuweka mipangilio ya faragha kwenye mitandao ya kijamii”,amesema Mhandisi Imelda.
Amefafanua kuwa TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu na wanaendelea kutoa elimu ili watumiaji wote wa mtandao wanakuwa salama bila kuwaacha nyuma watu wenye ulemavu ili kuhakikisha wanapata haki sawa za usalama wa taarifa binafsi.
Ameongeza kuwa, TCRA ina wajibu wa kuwalinda watumiaji wote wa mtandao na kupitia juhudi hizi, tunahakikisha watu wenye ulemavu wanaweza kutumia mtandao kwa usalama na bila wasiwasi wa kukumbana na uhalifu au ukiukwaji wa haki zao na imeendelea kutoa njia za kuripoti uhalifu na matukio ya hatari mtandaoni kama vile uonevu, udanganyifu au utapeli.
Akielezea njia za kuwa salama mtandaoni amesema ni pamoja na kuepuka kutoa taarifa za kibinafsi kwa watu usiofahamu na kutumia njia salama za malipo mtandaoni.
“Usiruhusu kitambulisho chako cha NIDA kumsajilia mtu mwingine laini ya simu na usimpatie mtu yoyote namba ya siri (PIN) ya pesa. Kwenye masuala ya mtandao hakuna mambo ya mwili mmoja ndiyo maana kila mtu anasajili kwa kutumia namba yake ya NIDA. Hakiki namba zako kupitia *106# ”,ameeleza Mhandisi Imelda.
Aidha amewashauri watumiaji wa mtandao kulinda taarifa zao kwa kutumia nywila (neno la siri) thabiti akisisitiza kutumia neno la siri tofauti kwa kila akaunti
“Pia tuwaelimishe watoto juu ya hatari zilizomo kwenye mtandao na jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa usalama. Tunza faragha yako binafsi pamoja na ile ya familia yako, epuka kuweka kwenye mtandao wa kijamii taarifa binafsi kwa kina. Achana na mambo ya kuweka kila kitu chako mtandaoni, kuweka taarifa zako nyingi mtandaoni ni hatari”,ameongeza Mhandisi Imelda.
“Usitekeleze maelekezo yoyote kutoka kwa mtu anayejitambulisha kuwa mtoa huduma ikiwa amekupigia kwa namba ya kawaida kwani Mtoa huduma wako wa mtandao wa simu atawasiliana na wewe kwa namba 100 pekee”,ameeleza.
“Ni rahisi sana kumtambua tapeli kwani atakupigia namba ya kawaida badala ya namba 100, Ni rahisi sana kutoa taarifa kwa mtu anayetaka kukutapeli tuma namba yake kwenye namba 15040. Ni rahisi sana kuwasiliana na TCRA endapo una malalamiko yanayomhusu mtoa huduma wako au ukitaka kupata elimu au ushauri wa kutaka kuanzisha biashara ya mawasiliano piga namba ya bure 0800008272”,amesisitiza Mhandisi Imelda.
Aidha ameshauri wahakikishe program za kifaa cha mawasiliano zimeboreshwa (Updated) zimesasishwa.
“Punguza uharaka unapotuma pesa, hakiki namba unayotaka kuitumia pesa. Kabla ya kufanya malipo au kununua bidhaa mtandaoni, hakikisha taarifa za mtu unayemlipa au tumia huduma ya wakala aliyesajiliwa. Usitume pesa kabla ya kupokea mzigo au kuwa na mawasiliano ya uhakika ili kulinda usalama wa pesa zako, usiwe na haraka”,amesema.
“Epuka kufungua fungua, kubofya viunganishi (links) usivyovifahamu mtandaoni, jiepushe ili kulinda taarifa zako na ukihisi akaunti yako imeingiliwa au kudukuliwa (Hacked) toa taarifa kwa jeshi la polisi”,amesema Mhandisi Imelda.
Aidha amewataka watumiaji wa mtandao kuepuka kusambaza mtandaoni maudhui yaliyokatazwa kama vile udhalilishaji, uongo, uchochezi au upotoshaji lakini pia wahakikishe kabla ya kusambaza taarifa, wajiridhishe kama ni za kweli na zimethibitishwa kutoka chanzo rasmi kama vile chombo cha habari rasmi au ukurasa rasmi wa taasisi.
“Epuka kusambaza maudhui ya ngono mtandaoni kwa sababu inaweza kusababisha madhara kwa watoto na kuharibu mahusiano. Usikubali kutuma picha za utupu hata kama unampenda kiasi gani. Lile wazo la kupiga picha za utupu, unapiga ili iweje, unazipakua, unazitunza za kazi gani? Huu ni ushetani. Tuwe makini haya mambo ni hatari usiombe yakukute mtu kasambaza picha zako za utupu”,ameongeza.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo na kuomba kuendelea kutoa elimu zaidi ili watumiaji wa mitandao wawe salama zaidi.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Oktoba 17,2024 Mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (katikati) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (katikati) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Ansila Joackim Materu akizungumza wakati TCRA ikitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao