Breaking

Wednesday, 30 October 2024

RAS KATAVI AIPA HEKO TANROADS KWA MAFUNZO YA WATUMISHI WA MIZANI

Na Mwandishi Wetu,Katavi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela amewapongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuendesha mafunzo ya sheria ya uzito wa magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa watumishi wake wa Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora, Rukwa, Kigoma na wenyeji Katavi.

Msovela amesema kuwa mafunzo haya ambayo pia yatawezweshwa na wakufunzi kutoka Wizara ya Ujenzi, yatawajengea uwezo watumishi hawa na kuwa makini katika utendaji wao wa kazi kutokana na kuwahudumia wasafirishaji wa ndani na nje ya nchi, ambao baadhi yao wanazifahamu vema sheria za uzito wa magari.

“Ninaimani baada ya mafunzo haya watumishi hawa watatoka wanaijua vyema hii sheria, na watatenda sawasawa na sheria hii bila kuipindisha wakijua wazi wanazilinda barabara zetu na uharibifu wa magari yenye kujaza mizigo aidha kwa makusudi au kutokujua,” amesema Msovela.

Hatahivyo, amewataka watumishi hao kuwa wazalendo, waandilifu na waaminifu siku zote wanavyofanya kazi kwenye mizani, itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara na matengenezo ya mara kwa mara.

Ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinui ya barabara kwa kiwango cha lami, ambapo ssa kila kona ya nchi inafikika vizuri na kwa muda mfupi, tofauti na miaka ya nyuma barabara nyingi ikiwemo ya Katavi ilikuwa mbovu na yenye mashimo mengi, na kusababisha usafiri na usafirishaji kuwa mgumu pia.

Halikalidhalika, amewataka baadhi ya wasafirishaji ambao sio waaminifu kuacha tabia za kuzidisha uzito kwenye magari yao kwa makusudi, bila kujali miundombinu inayojengwa kwa gharama kubwa, kwani ni kosa la kisheria na wataadhibiwa kwa kulipishwa faini, au kifungo au vyote kwa pamoja.

“Sio neno zuri kulitumia wasafirishaji wanatapisha wakishajaza wanajaza aidha mizigo au abiria na wakifika karibu na mizani wanatumia magari madogo na kupunguza mizigo na abiria na baada ya kuoita kwenye mizani wanarudisha kwenye magari na kuendelea.

Kwa upande wake Lawrence Boaz, Afisa Mizani kutoka Kigoma amesema watapata manufaa makubwa kwa kupata mafunzo haya na atakwenda kuwaelimisha wenzake ili waweze kwenda na sheria hii.

Naye Martha Soka, msimamizi wa mizani kituo kwa Kamsisi mkoa wa Katavi, amesema mafunzo haya yamemjengea uwezo kwa kwenda kuelimisha wasafirishaji wanaozidisha mizigo.








Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages