Breaking

Monday, 14 October 2024

RAIS SAMIA ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA KUMBUKIZI YA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wengine mbalimbali, wananchi na waumini wakati akishiriki ibada ya Misa Takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Fransisko Ksaveri- Nyakahoja jijini Mwanza, leo tarehe 14 Oktoba, 2024.

Viongozi wengine walioshiriki ibada hiyp pamoja na Mhe. Rais Dkt. Samia, ni pamoja na Mhe. Dkt. Phillip Isdory Mpango, Makamu wa Rais ws Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Hussen Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu.










Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages