Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyaelekeza makampuni ya madini kuchangia na kushirikiana na chuo cha VETA Geita katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi.
Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo hayo alipotembelea wakati akifunga Maonyesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini, jana, tarehe 13 Oktoba, 2024.
Mhe. Rais amesema ushirikiano huo pia uwawezeshe vijana kujifunza na baada ya kuhitimu wafanye kazi kwenye makampuni ya madini yaliyopo ndani ya mkoa wa Geita.
Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Martin Shigella kuratibu suala hilo na kuhakikisha linatekelezwa.