Breaking

Monday, 7 October 2024

MARIAM ULEGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI NGOKOLO

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (kushoto) akikabidhi Taulo za kike kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mwalimu wa Ushauri Nasaha na Malezi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, Martha Moses.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake  wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega ametoa msaada wa Taulo za kike kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati akikabidhi Taulo za kike katika shule hiyo leo Jumatatu Oktoba 7,2024 Mariam amesema taulo hizo, zitawasaidia wanafunzi kujistiri wakati wa hedhi hivyo kuzingatia zaidi masomo yao.

Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kwa malengo hivyo wajiepushe na vishawishi vinavyoweza kukwamisha ndoto zao.

“Nimekuja kuwaona watoto wa kike katika shule hii, nimewaletea zawadi kidogo ili muweze kujistiri wanangu, mimi nawapenda sana, nawatakia masomo mema. Elimu ndiyo ufunguo wa maisha , elimu ina matunda makubwa sana niwaombeni sana msome kwa bidii lakini katika bidii hiyo msome kwa malengo, wakataeni wale wanaokuja kwa malengo ya kuwaharibia maisha”,amesema Mariam.

“Najua kuna mambo ya ukatili wa kijinsia, naomba mpinge vikali sana  vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia, Mtoto wa kike jitambue soma kwa bidii, hakikisha unatimiza malengo yako.  Sasa hivi wanawake wote, watanzania wote, dunia nzima mfano wetu wa kuigwa ni Mhe. Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyinyi ni mama Samia wa kesho, someni ili mfikie malengo yale mnayataka”,ameongeza Mariam.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Ushauri Nasaha na Malezi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, Martha Moses ameshukuru Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa  UWT Taifa, Mariam Abdallah Ulega kwa kuwapatia zawadi ya taulo za kike wanafunzi wa shule hiyo huku Makamu Mkuu wa Shule hiyo Mponda Martine akiwaomba wadau kuendelea kutembelea shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1415 ambayo sasa inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo, yaliyopo ni matundu 12 tu.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (kushoto) akikabidhi Taulo za kike kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 7,2024. Kulia ni Mwalimu wa Ushauri Nasaha na Malezi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, Martha Moses - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa sehemu ya maboksi yenye taulo za kike zilizotolewa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah  kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (kulia) akikabidhi Taulo za kike kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (katikati) akikabidhi Taulo za kike kwa wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega akizungumza na wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (katikati) akisalimiana na wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (katikati) akisalimiana na wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (katikati) akiwa na wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, Ndugu Mariam Abdallah Ulega (katikati) akiwa na wasichana wanaosoma katika Shule ya Sekondari Ngokolo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Mponda Martine akielezea kuhusu changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages