Breaking

Tuesday, 22 October 2024

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA OFISI YA RAIS UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Abeid Ramadhani (katikati) akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Magufuli (kushoto) kabla ya kuingia katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024 kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi kwa wakati sahihi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo jijini Dodoma kwa niaba ya kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

“Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesheheni wabobezi wa sekta zote jambo linalowafanya watendaji wa ofisi hii pamoja na taasisi zilizopo chini yake kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Mhe. Dkt. Mhagama amesema.

Aidha Dkt. Mhagama ameishukuru Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa kamati hiyo kwani wajumbe wake wamekuwa wakipatiwa uelewa mpana juu ya utekelezaji wa majukumu ya kila taasisi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Mhagama ameishauri Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora kutoa mrejesho mara kwa mara kwa wananchi juu ya hatua mbalimbali ambazo imekuwa ikizichukua na kuzifanyia kazi baada ya kupokea malalamiko au changamoto ya masuala mbalimbali ili kuonesha namna ambavyo ofisi hiyo imekuwa ikiwajibika na kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itapokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa siku mbili, tarehe 21 na 22 Oktoba, 2024.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages